Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Pius Stephen Chaya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Mashariki

Primary Question

MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza: - Je, jitihada gani zimefanyika kurahisisha upatikanaji wa visa kwa watalii wenye uraia tofauti wanaokuja nchini kwa mwitikio wa Royal Tour?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninayo maswali mawili ya nyongeza; swali la kwanza, kwa kuwa Tanzania tuna urithi mkubwa wa utamaduni wa asili, hususani Mikoa ya Singida na Dodoma, je, nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kwamba tuna promote utalii wa utamaduni kwa mikoa ya Singida na Dodoma?

Swali la pili, Manyoni katika Tarafa ya Kilimatinde ilikuwa ni route ya watumwa, sasa je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba tunaboresha mali kale ya Kilimatinde ili iweze kutumika kwa ajili ya utalii? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli Taifa letu lina utajili wa mila, desturi, tamaduni na maeneo ya kiutamaduni ambayo yanafaa kutembelewa, lakini vilevile tuna utajili wa vyakula vingi katika nchi yetu kutokana na uwepo wa makabila zaidi ya 120. Kwa kulitambua hili Serikali imekuwa ikifanya mikakati ya kushirikiana na mikoa mbalimbali kukutana na wadau katika mikoa hiyo, kwanza kuainisha maeneo haya ambayo yanaweza kuwa vivutio vya utalii, lakini pili kuainisha aina ya vyakula ambavyo vinaweza kutumika kutangaza utalii kwenye maeneo yetu. Hivi tunavyozungumza kuna matamasha yanaendelea ya utalii (cultural tourism) katika Mkoa wa Dodoma, ambayo yanahusisha vilevile kutembelea mashamba ya zabibu na kuangalia vikundi vya utamaduni, lakini vilevile kupata fursa ya kuona mila na tamaduni za Mkoa wa Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Mkoa wa Singida tayari tuna mawasiliano na wenzetu wa Dodoma, tunakusudia kuwa na kongamano kubwa na wadau wa utalii katika mkoa ule ili kuweza kuainisha kwa pamoja vivutio hivi na kuona jinsi ambavyo tunaweza ku-promote cultural tourism katika Mkoa wa Singida.

Mheshimiwa Spika, kwenye eneo hili la pili kuhusiana na vivutio vya utalii kule Manyoni, ni kweli timu yetu ilishakwenda katika Wilaya ya Manyoni na kwa Mkoa wa Singida kwa ujumla, tuna maeneo ambayo tumeyabaini kama vivutio, yapo maeneo ambayo yanamilikiwa na Kanisa Anglikana, yapo maeneo ambayo kuna Boma la Kale la Mjerumani lakini vilevile ipo njia ile ya kati ya watumwa kwenye maeneo ya Kilimatinde. Maeneo haya yote tumekwishayabaini, sasa tunachofanya ni tunampango wa kukaa na hao wadau katika eneo lile ili kukubaliana yale ambayo wanayamiliki kisheria tuone jinsi ambavyo tunaweza kuyatangaza kwa pamoja na yale ambayo wapo tayari kuyaachia ili Serikali iweze kuyasimamia tutafanya hivyo. (Makofi)