Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Neema William Mgaya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA W. MGAYA K.n.y. MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: - Je, jitihada zipi zinafanywa na Serikali kuhakikisha Wilaya ya Ludewa inajengewa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji?

Supplementary Question 1

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa kuwa Mkoa wa Njombe ni wakulima wazuri wa zao la chai, je, Serikali mmejipanga vipi kuhakikisha kwamba mnaweka miundombinu rafiki kwa wakulima wadogo wadogo wa chai ili chai ile iweze kuleta tija kwa wakulima hawa wadogo wadogo? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, nimthibitishie tu Mheshimiwa Mbunge, dada yangu Neema kwamba moja ya mkakati wa Serikali tulionao sasa hivi ni kuchimba visima 67,000 kwa wakulima wadogo wadogo nchini na kazi hiyo tunatarajia kuanza hivi karibuni ikiwemo katika Mkoa wa Njombe ambapo tumeshuhudia wiki mbili zilizopita tumepokea magari kwa ajili ya uchimbaji na magari yale yatafanya kazi hizo ikiwemo Mkoa wa Njombe kwenye kila zao.

Kwa hiyo, tutafanya kwenye chai, kwenye kahawa mazao karibu yote ambayo yanamgusa moja kwa moja mkulima mdogo. Kwa hiyo lipo katika mpango wetu na nimthibitishie litafanyika hivyo, ahsante.

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA W. MGAYA K.n.y. MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: - Je, jitihada zipi zinafanywa na Serikali kuhakikisha Wilaya ya Ludewa inajengewa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji?

Supplementary Question 2

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Kwa kuwa Wilaya Rungwe inapata mvua zaidi ya miezi nane lakini miezi minne inayobaki inakuwa ni ya jua na sisi ni wakulima wazuri sana wa chai na parachichi, umesema mmepata magari na mtayapeleka Njombe.

Mheshimiwa Spika, Serikali inasema nini juu ya Wilaya ya Rungwe kuhakikisha magari yanafika kwa kuwa na sisi ni wakulima wazuri? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante, nimesema tutachimba mikoa yote nchini ikiwemo Mkoa wa Njombe na idadi ya visima tutakavyochimba ni 67,000 na magari yameshafika na tutafanya operation, tutakuwa tunavamia mkoa mmoja tunachimba tunamaliza, tunakwenda mkoa mwingine, hatutafanya kazi nusunusu. Kwa hiyo, hata Rungwe, Mkoa wa Mbeya tutafika, hata Songwe kule ninakotokea na kwenyewe tutafika, ahsante. (Makofi)