Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Grace Victor Tendega
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza: Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha uvunaji wa maji ya mvua unapunguza changamoto ya maji?
Supplementary Question 1
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali kwamba mmejenga mabwawa zaidi ya 45 na mengine 19 mnaendelea kuyafanyia kazi lakini katika maeneo ya zahanati, katika vituo vya afya na katika hospitali mbalimbali kumekuwa na changamoto kubwa sana ya maji.
Je, Serikali hamuoni haja sasa ya kujenga miundombinu kwa ajili ya uvunaji wa maji katika maeneo hayo? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, mikoa iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini ikiwepo Mkoa wa Iringa ni mikoa ambayo inapata mvua kwa miezi minne hadi minane na wakati wa mvua maji hutiririka na yakaenda kwenye mito mikubwa na kadhalika, lakini katika Jimbo la Kalenga bado kuna changamoto ya maji, mvua zikinyesha maji yanakuwepo yanatiririka yanaenda yanapotea.
Mheshimiwa Spika, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba maji hayo yanatengenezewa mabwawa katika Jimbo la Kalenga kwa mfano, Kata ya Luhota katika eneo Kijiji cha Kitayawa kuna mto huwa unatokea wakati wa mvua lakini mvua ikiondoka wanapata adha ya maji? Ahsante. (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, pia namshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa swali zuri kabisa, lakini pia ni kwamba kama ambavyo nimejibu katika majibu yangu ya msingi, Serikali tayari imejenga mabwawa 45, 19 yanaendelea.
Mheshimiwa Spika, maendeleo ni hatua kwa hatua na maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja Serikali tunayachukua kwa ajili ya kuna namna ambavyo kadiri upatikanaji wa fedha utakaporuhusu tutajenga specific katika katika eneo la Kalenga kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameshauri.
Mheshimiwa Spika, katika upande wa kujenga miundombinu rafiki ya uvunaji wa maji katika shule na taasisi nyingine mbalimbali kama ambavyo pia nimejibu katika majibu ya msingi, ni mkakati wa Serikali kuendelea kujenga, lakini kuboresha pale ambapo tayari miundombinu na pale ambapo tunaona kwamba kuna changamoto zaidi basi Serikali itaendelea kuwekeza fedha lengo kubwa ni kuendelea kuhakikisha kwamba maji ambayo yanapatikana yanatokana na mvua tuendelee kuyavuna na hatimaye yatasaidia katika kutatua katika upungufu wa maji na vilevile kuzuia uharibifu wa miundombinu katika maeneo ya shule au taasisi nyinginezo ambazo zinatokana na maji kutiririka hovyo, ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved