Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza: - Je, lini maji kutoka Ziwa Victoria yatafika katika Vijiji vya Sirari, Nyamwaga na Nyamongo vilivyopo Tarime Vijijini?

Supplementary Question 1

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, tenki limejengwa Sirari, Mogabiri na pale Komaswa, naomba nijue uhakika wa Serikali na hasa Wizara ya Maji kuweka matoleo pale Sirari, Mogabiri na Komaswa ili wananchi hao wa Ganyange, Nyamwaga na Nyamongo wawe na uhakika kwamba kwa awamu ijayo watapata maji kutoka Ziwa Victoria?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mradi wa Maji Korotambe na Masanga ulichibwa maji yakaanza kutoka sasa umekwama. Nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba watu wa Korotambe, Masanga, Masurura, Kitawasi wanakunywa maji ya bomba kama ambavyo waliaminishwa hapo mwanzo? Ahsante. (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, ni kweli kabisa mradi wetu huu na matenki yamejengwa pale Sirari na Mogabiri, lakini kuna maeneo ambayo tunafanya usanifu katika mwaka wa fedha 2025/2026 ili kuhakikisha kwamba maeneo ya Komaswa na Sirari tunayahakikishia kwamba Serikali hilo tumeshalipokea na Mheshimiwa Mbunge si mara ya kwanza kuliongelea siyo ndani ya Bunge lakini amekuwa akilifuatilia sana kwa kina hili suala na sisi tumeshalichukua na linaingizwa katika usanifu utakaofanyika katika mwaka wa fedha 2025/2026 kuhakikisha kwamba matoleo katika upande wa komaswa na wao wanaenda kupata maji ya Ziwa Victoria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Mradi wa Masanga, tulikuwa na kisima ambacho kilikuwa na uwezo wa kutoa maji lita 6,000 kwa saa, lakini kwa bahati mbaya kikapoteza uwezo wake wa kuzalisha maji na sasa kinazalisha takribani 1,500 ambayo hayawezi kutosheleza katika maeneo yote. Kwa hiyo, sisi tunachokifanya sasa ni kutumia ile miradi inayofanyika katika maeneo ya jirani ya Nyanungu, nafikiri kuna eneo Nyanungu pale ambapo ule mradi utakapokamilika ndio tutafanya extension kwa ajili ya kuja kuhudumia maeneo ya Masanga.

Mheshimiwa Spika, vilevile katika mradi ambao Korotambe, maeneo ya Korotambe tulikuwa tunatumia jenereta, ule mradi baada ya jenereta kuzidiwa ikabidi sasa tufanye utaratibu wa kubadilisha mifumo ambayo ilikuwa inasaidia ku-pump maji kwenda katika umeme wa TANESCO na sasa tayari mkandarasi yupo site anaendelea kuhakikisha kwamba maeneo mengi siyo kwa Korotambe pekee yake na yale maeneo mengine ambayo yanazunguka katika eneo hilo ambayo yalikuwa yananufaika na mradi huo. Lengo ni kwamba waendelee kupata huduma ya maji safi na salama, ahsante sana. (Makofi)

Name

Leah Jeremiah Komanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Meatu

Primary Question

MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza: - Je, lini maji kutoka Ziwa Victoria yatafika katika Vijiji vya Sirari, Nyamwaga na Nyamongo vilivyopo Tarime Vijijini?

Supplementary Question 2

MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Je, ni lini Serikali itapeleka maji ya Ziwa Victoria katika Jimbo la Meatu ili kuweza kukabiliana na athari ya mabadiliko ya tabianchi? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na namshukuru sana dada yangu Mheshimiwa Leah Komanya, Mbunge wa Meatu kwa kazi nzuri ambayo kwa kushirikiana na Wabunge wa Mkoa wa Simiyu kwa kuhakikisha kwamba umesemewa mradi huu kikamilifu na Mheshimiwa Rais alishatoa fedha takribani shilingi bilioni 440 kwa ajili ya kuyatoa maji kutoka Nyashimo, Bariadi kwenda Itilima na sasa tupo katika awamu ya pili mradi wa kwanza upo 20% na mradi wa pili ambako sasa itaanza Maswa kwenda mpaka Meatu. Kwa hiyo, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge awamu ya pili hii inaenda kufika mpaka Meatu. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Deo Kasenyenda Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makambako

Primary Question

MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza: - Je, lini maji kutoka Ziwa Victoria yatafika katika Vijiji vya Sirari, Nyamwaga na Nyamongo vilivyopo Tarime Vijijini?

Supplementary Question 3

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kuniona, Mji wa Makambako wananchi wanapata shida sana suala la maji; je, Serikali imejipangaje kuhakikisha inaondoa tatizo la maji katika Mji wa Makambako? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na namshukuru sana kaka yangu kwa kazi nzuri anayofanya kwa ajili ya wananchi wake wa Makambako na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliridhia kutoa kiasi cha shilingi bilioni 42 kwa ajili ya kupeleka kwenye Mradi wa Miji 28 ambapo mpaka sasa mradi huu umeshafikia 20% na tunaamini kwamba mradi huu utakapokamilika Mji wa Makambako suala la maji halitokuwa tatizo tena, ahsante sana. (Makofi)

Name

Boniphace Nyangindu Butondo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kishapu

Primary Question

MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza: - Je, lini maji kutoka Ziwa Victoria yatafika katika Vijiji vya Sirari, Nyamwaga na Nyamongo vilivyopo Tarime Vijijini?

Supplementary Question 4

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, upembuzi yakinifu umefanyika katika Kata za Seke Bugoro, Mondo, Mwasubi na Bunambiyu; je, Serikali iko tayari sasa kupeleka shilingi bilioni 16.5 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu?
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Spika, je, Serikali iko tayari kupeleka shilingi bilioni 16.5 ambazo zimeonekana katika zoezi la upembuzi yakinifu na wa kina kwa ajili ya utelezaji wa miradi katika kata hizo? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana nashukuru pia Mheshimiwa Butondo kwa kazi nzuri aliyoifanya na kwa kushirikiana na Serikali mpaka tukafanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ambao ikatupatia gharama ya shilingi bilioni 16.5. Serikali iko tayari kwa ajili ya kwenda kuhakikisha mradi huo unatekelezwa. (Makofi)

Name

Prof. Patrick Alois Ndakidemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Vijijini

Primary Question

MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza: - Je, lini maji kutoka Ziwa Victoria yatafika katika Vijiji vya Sirari, Nyamwaga na Nyamongo vilivyopo Tarime Vijijini?

Supplementary Question 5

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, baadhi ya maeneo katika Vijiji vya Sango, Shia, Mdawi na Kisaseni katika Kata ya Kimochi yana uhaba mkubwa sana wa maji; je, Serikali ina mikakati kupeleka maji katika maeneo haya? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na namshukuru sana Mheshimiwa Profesa Ndakidemi, Mbunge wa Moshi Vijijini, lakini lazima niseme jambo moja hapa kwamba Kata ya Kimochi, Serikali iliweka miundombinu na kwa bahati mbaya wananchi wa Kata hii ya Kimochi walihujumu miundombinu hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa Mheshimiwa Mbunge aliomba fedha na Serikali tumeshatoa shilingi milioni 983 na Mheshimiwa Mbunge ameshaomba nyingine tena shilingi milioni 484 lakini naomba tutoe maelekezo kwa wasimamizi wote wa vyanzo hivi na miundombinu wananchi wapewe elimu ya kutosha ili wasiendelee kuharibu miundombinu ni fedha ambazo ni za walipa kodi ambazo tunaamini kwamba wakisimamia hizi fedha zingeenda kufanya kazi nyingine. Serikali tuko tayari kuendelea kushirikiana na wananchi wa Moshi Vijijini, ahsante sana. (Makofi)

Name

Athumani Almas Maige

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Kaskazini

Primary Question

MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza: - Je, lini maji kutoka Ziwa Victoria yatafika katika Vijiji vya Sirari, Nyamwaga na Nyamongo vilivyopo Tarime Vijijini?

Supplementary Question 6

MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, Mradi wa Miji 28 unapeleka maji Urambo kupitia Uyui; je, lini Serikali itaanza maandalizi ya kupeleka maji katika Vijiji vya Mabama, Ilolangulu, Ufuluma na Ndono? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, ni kweli kabisa Serikali imeshapeleka maji Tabora kwa shilingi bilioni 680; imepeleka Urambo Kaliua pamoja maeneo mengine kwa shilingi bilioni 143 na sasa kazi iliyobaki ni kuendelea kufanya upanuzi wa mradi ili vijiji vingi zaidi viweze kufikiwa. Nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge na vijiji hivyo katika JIMBO lake la Uyui tutafikisha huduma hiyo. Nakushukuru sana. (Makofi)

Name

Selemani Moshi Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Vijijini

Primary Question

MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza: - Je, lini maji kutoka Ziwa Victoria yatafika katika Vijiji vya Sirari, Nyamwaga na Nyamongo vilivyopo Tarime Vijijini?

Supplementary Question 7

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, ahsante, Mradi wa Maji wa Kata ya Kapalamsenga umekwama kwa kukosa shilingi milioni 700 kukamilisha ujenzi wa matenki; ni lini Serikali itapeleka fedha hizo ili kukamilisha huo mradi? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, lakini pia namshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa kuendelea kukumbusha kwa sababu najua tumeendelea kuwasiliana kuhusu jambo hili na sisi Serikali tunalijukulia kwa uzito wake na Katibu Mkuu ameshaelekeza Mameneja wa Mikoa kuhakikisha kwamba wanaleta hati za madai ili tuhakikishe kwamba sasa wakandarasi wetu wanalipwa na ili warudi site ili wakaendelee na miradi ikamilike na wananchi wapate huduma ya maji safi na salama. Nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kazi hiyo tunaendelea nayo na naamini kwamba itakamilika muda si mrefu, ahsante sana. (Makofi)

Name

Felista Deogratius Njau

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza: - Je, lini maji kutoka Ziwa Victoria yatafika katika Vijiji vya Sirari, Nyamwaga na Nyamongo vilivyopo Tarime Vijijini?

Supplementary Question 8

MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, katika Kata ya Mbokomu yenye vitongoji 21, ni vitongoji nane tu ndio vinapata maji licha ya kuwa na miundombinu mizuri ya maji. Ni lini Serikali itaenda kuweka miundombinu ili vitongoji vingine viweze kupata maji? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na namshukuru sana dada yangu Mheshimiwa Felista Njau kwa kuwasemea wananchi katika vitongoji hivyo. Naomba nilipokee hili ili tukalichakate kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunaenda kutoa majibu stahiki yakiendana na utekekezaji husika, ahsante sana. (Makofi)