Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Francis Isack Mtinga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iramba Mashariki
Primary Question
MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami kilometa 42 barabara inayoelekea Makao Makuu ya Wilaya Mkalama?
Supplementary Question 1
MHE. FRANCIS I. MTINGA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, barabara hii tulipewa kilometa 10 tangu enzi Mheshimiwa Mbarawa akiwa Waziri wa Ujenzi na tumekuwa tukisubiri barabara hii kwa muda mrefu sana. Je, Serikali sasa inaweza ikasema ni lini itakwenda site Mkalama kwa ajili ya kujenga hizi kilometa 10 ambazo zimekuwa ni hadithi kwa Wana-Mkalama? Swali la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, inapopita barabara hii katika Kata za Iguguno, Kinyangiri, Nduguti, Gumanga, Ibaga mpaka kule Mpambala, wananchi wameondoa nyumba zao wamevunja kwa hiyari na katika hawa wananchi wapo wenye alama za X ya kijani kwa maana wanastahili kulipwa; pamoja na kuwa Serikali inachelewa kujenga barabara hii. Ni lini basi itawalipa wananchi hawa ambao wamebomoa nyumba zao ili waweze kuendelea na maisha yao wakati wa kisubiri lami hii ambayo haifiki? Ahsante. (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwanza, kwenda site Wizara iko tayari lakini kinachoendelea sasa hivi ni kwamba tukishakamilisha taratibu za ununuzi kwa maana mkandarasi amepatikana ndio atakwenda site na Wizara itakuwa tayari kumsimamia huyo mkandarasi ambaye atakuwa amepatikana na tupo kwenye hatua za mwisho kabisa za ununuzi.
Mheshimiwa Spika, kuhusu fidia ya hawa watu ambao watapisha ujenzi ama mradi nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tulishakamilisha tathmini na tulishapeleka maombi ya malipo ya fidia Wizara ya Fedha na kabla hatujaanza ujenzi tuna uhakika kwamba tutakuwa tumewalipa hao wananchi, ahsante.
Name
Yahya Ally Mhata
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyumbu
Primary Question
MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami kilometa 42 barabara inayoelekea Makao Makuu ya Wilaya Mkalama?
Supplementary Question 2
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Spika, ahsante, mkandarasi anayeweka taa za barabarani katika Jimbo langu la Nanyumbu amesimamisha huduma hiyo kwa kukosa malipo; je, ni lini mkandarasi huyo atalipwa ili aendelee na kazi hiyo ya uwekaji wa taa? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba nikubaliane na Mheshimiwa Mbunge na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tumeshatoa hati za malipo kwa maana hati za madai za mkandarasi Hazina ili waweze kumlipa huyo mkandarasi na aweze kuendela na kazi ya kukamilisha uwekaji wa hizo taa, ahsante. (Makofi)
Name
Josephine Johnson Genzabuke
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami kilometa 42 barabara inayoelekea Makao Makuu ya Wilaya Mkalama?
Supplementary Question 3
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Spika, ahsante, je, ni lini Serikali itajenga barabara ya kutoka Buhigwe – Katundu- Heru Ushingo mpaka Kitanga kwa kiwango cha lami? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, Mheshimiwa Spika, samahani.
Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba barabara aliyotaja iko Mkoa wa Kigoma ambayo ni barabara ya ulinzi na tunavyoongea sasa hivi kitu cha kwanza ni kujenga kwanza daraja la kuunganisha Wilaya ya Kasulu na Kibondo halafu tukamilishe usanifu na kwa sababu kipaumbele pia ni barabara za ulinzi. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge baada ya kukamilisha daraja ambalo litakuwa na uwezo wa kuunganisha sasa tutaanza mipango ya kuijenga hiyo barabara kwa kiwango cha lami, ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Primary Question
MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami kilometa 42 barabara inayoelekea Makao Makuu ya Wilaya Mkalama?
Supplementary Question 4
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Spika, ahsante, ni lini Serikali itakamilisha Barabara ya Nyakato – VETA - Buswelu mpaka Igombe TX yenye kilometa 18.2 imebakia kilometa nne na imejengwa kwa miaka 10 sasa bila kukamilika?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, dhamira ya Serikali ni kukamilisha hiyo barabara yote kwa kiwango cha lami na hasa ikizingatiwa ukuwaji wa kasi wa Mji wa Mwanza. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mipango yetu ya mwaka unaokuja wa fedha tumepanga hiyo barabara ili iweze kujengwa na kukamilika, ahsante. (Makofi)
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Primary Question
MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami kilometa 42 barabara inayoelekea Makao Makuu ya Wilaya Mkalama?
Supplementary Question 5
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, je, ni lini Serikali itamlipa mkandarasi ambaye anajenga barabara ya kimkakati ya Matai kwenda Kasesha border ambaye sasa hivi hayupo kwa sababu hajalipwa fedha?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, Barabara ya Matai - Kasesya ni kati ya barabara ambazo tumeshapata wakandarasi lakini wanasubiri kulipwa fedha za awali. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kama Serikali tumeshawasilisha mahitaji ama madai ya mkandarasi kwa ajili ya advance payment na tuna uhakika akishalipwa mkandarasi huyo ataanza kazi ya kujenga ili kuunganisha Tanzania na Zambia kupitia mpaka wa Kasesya, ahsante. (Makofi)
Name
Elibariki Emmanuel Kingu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Magharibi
Primary Question
MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami kilometa 42 barabara inayoelekea Makao Makuu ya Wilaya Mkalama?
Supplementary Question 6
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, Barabara ya Singida – Sepuka – Ndago mpaka Kizaga inajengwa kwa kusuasua licha ya mkandarasi kulipwa advance payment kwa muda wa miezi karibia minne sasa. Nini kauli ya Serikali kuhakikisha mkandarasi huyu anatimiza wajibu wa kujenga barabara hii kwa speed inayotakiwa?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, ni kweli na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tumeshamwelekeza Meneja wa Mkoa ambaye anasimamia mkandarasi huyu kwa ukaribu kwamba baada ya kukamilisha taratibu zote za maandalizi ya awali aweze kuongeza kasi ili barabara hii muhimu sana iweze kukamilishwa. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Singida kwamba hiyo barabara tutahakikisha kwamba inakamilika kwa muda, ahsante.
Name
Eng. Stella Martin Manyanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nyasa
Primary Question
MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami kilometa 42 barabara inayoelekea Makao Makuu ya Wilaya Mkalama?
Supplementary Question 7
MHE. DKT. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa kuwa Serikali imekuwa ikifanya matengenezo ya mara kwa mara kwenye eneo takribani kilometa 15 kutoka Mbamba Bay, eneo la Luika Ngindo ambapo kila mwaka maji yanakuwa mengi hapo kiasi kwamba magari yanalala jambo ambalo kwa siku hizi kwa kweli ni aibu kwa jinsi ambavyo Serikali imefanya kazi vizuri.
Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba eneo hilo litengenezwe kwa kiwango cha lami kwa kutumia upembuzi yakinifu ambao tayari umeshafanyika katika barabara hiyo?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU SPIKA WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, niseme tu kwamba katika mwaka huu wa fedha, fedha nyingi sana imepelekwa kwenye maeneo ambayo yalikuwa na changamoto na hasa kipindi cha mvua na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba naomba nilichukuwe hili suala kwa sababu maeneo yote yaliyokuwa na changamoto tuliweza kuyapangia fedha ili kuyadhibiti wakati wa mvua iweze kupitika.
Mheshimiwa Spika, niombe kuchukuwa suala la Mheshimiwa Mbunge, lakini pia nimuagize Meneja wa Mkoa wa Ruvuma aweze kwenda kwenye hilo eneo afanye tathmini na aweze kuleta mapendekezo yake Wizarani ili tuone namna ya kufanya ili kuondoa adha ambayo inawakuta wananchi hao, ahsante.