Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Benaya Liuka Kapinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Vijijini

Primary Question

MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza upembuzi yakinifu na kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Nyoni – Maguu?

Supplementary Question 1

MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Spika, ahsante, nishukuru kwa majibu ya Serikali.

Kwa kuwa barabara hii ni barabara pekee inayounganisha Tarafa ya Hagati na barabara kubwa inayoelekea mjini, lakini barabara hii huwa inagemka sana hasa kule chini kutokana na hali ya udongo uliopo wa tifutifu, je, Serikali ipo tayari kuharakisha mpango wake iweze kuijenga barabara hii?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kipande cha Luanda hadi Lituhi tayari tulipata mkandarasi toka mwaka jana na tayari mmesaini, lakini mpaka leo mkandarasi huyu hajaanza kazi kwa sababu hajapata advance, ni lini Serikali itampa advance barabara hii ianze kujengwa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika jibu langu la msingi kulingana na jiografia na hali halisi ya udongo wa jimbo la Mheshimiwa na hasa huko ambako hii barabara inapita ndiyo maana katika jibu langu la msingi tumesema tumeangalia yale maeneo yote korofi, kuyajenga ama kwa lami ama kwa zege pamoja na kwamba hiyo barabara bado ni rough road, lakini tumeliona hilo na niwahakikishie kwamba tutaendelea kufanya hivyo wakati tunaendelea kukamilisha usanifu ili tuweze kuondoa adha ambayo inatokea hasa kipindi cha mvua.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la Barabara ya Luanda – Lituhi - Ndumbi Port, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tulishasaini mkataba, tulishapeleka hati za madai kwa maana ya malipo ya awali ili mkandarasi huyo alipwe na aanze kazi ya ujenzi barabara yote hiyo ya Luanda – Lituhi – Ndumbi, ahsante.

Name

Jonas Van Zeeland

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mvomero

Primary Question

MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza upembuzi yakinifu na kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Nyoni – Maguu?

Supplementary Question 2

MHE. JONAS V. ZEELAND: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, barabara ya kutoka Lusanga kwenda Kibati ni barabara muhimu sana kwa uchumi wa nchi kwa sababu inaunganisha Mkoa wa Tanga na Morogoro; je, Serikali haioni sasa kuna haja ya kufanya upembuzi yakinifu ili barabara hii iweze kujengwa kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, ni kweli kwamba hiyo barabara aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge ni muhimu sana ambayo inaunganisha Mkoa wa Morogoro na Tanga na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba itakuwepo kwenye mpango wa usanifu, lakini kwa sasa tutakachohakikisha ni kwamba tunaitengea fedha iweze kukarabatiwa ili iweze kupitika kipindi chote wakati tunafanya maandalizi ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, ahsante.

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Primary Question

MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza upembuzi yakinifu na kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Nyoni – Maguu?

Supplementary Question 3

MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Spika, ahsante, Barabara ya Mahenje – Ndolezi – Hasamba kupitia Kilimampimbi – Iboya Serikali ilishafanya upembuzi yakinifu lakini kuna kipande kilichobaki; ni lini Serikali itakamilisha upembuzi yakinifu wa kipande cha Hasamba – Kilimampimbi – Iboya?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, tulishaanza hiyo kazi ya kufanya upembuzi yakinifu wa hiyo barabara na inasimamiwa na Mkoa wa Songwe. Naomba nimwelekeze meneja kuhakikisha kwamba katika mwaka wa fedha unaokuja kazi hiyo inakamilika ili tuweze sasa kuanza usanifu wa kina, ahsante.

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza upembuzi yakinifu na kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Nyoni – Maguu?

Supplementary Question 4

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, Halmashauri ya Mji wa Bunda inakuwa na ina barabara moja tu ya lami ya kwenda kwa Mkuu wa Mkoa, ni lini sasa Serikali mtatujengea lami kwenye mitaa yetu ya Mji wa Bunda ili na wenyewe uwe na hadhi na kufanana kama miji mingine?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ester Bulaya kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba tuna wakala mbili, TANROADS na TARURA, kwa hiyo barabara nyingi ambazo zinajengwa ambazo sio kubwa kwa maana ya Regional Roads zinajengwa na TANROADS na zile nyingi ambazo ni za miji huwa zinasimamiwa na TARURA. Naomba nichukuwe suala hili, sisi kama tuta-qualify kujengwa na TANROADS tuweze kufanya hiyo kazi, lakini kama zitakuwa ni za wenzetu wa TARURA basi nilichukuwe hilo ili Serikali iweze kuangalia na kufanya huo mji uwe na barabara za kiwango cha lami, ahsante.

Name

Priscus Jacob Tarimo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Mjini

Primary Question

MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza upembuzi yakinifu na kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Nyoni – Maguu?

Supplementary Question 5

MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana, Barabara ya Holili – Moshi – Arusha ni barabara ya muhimu sana kwa uchumi wa nchi hii na ina msongamano mkubwa sana, niishukuru Serikali imeshatoa fedha kwa vipande vitatu, Tengeru, Arusha National Park Junction, Kikafu pamoja na pale Moshi Mjini Maili Sita mpaka Kiboriloni, ni lini tutapata fedha kwa ajili ya upanuzi wa vipande vingine vyote vilivyobaki?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, nishukuru tu kwamba Mheshimiwa Mbunge anatambua tumeshapata fedha kwa hivyo vipande vitatu lakini pia ni barabara ambayo tunakwenda kujenga njia nne ikiwa ni pamoja na daraja na kwa kufanya hivyo, maana yake ni kuwa Serikali pia tunajipanga kujenga barabara yote kwenye kiwango hicho ili kupunguza msongamano mkubwa ambao upo katika hiyo barabara ya Arusha – Moshi – Holili, ahsante.