Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. HAWA M. CHAKOMA Aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kilindoni – Rasimkumbi - Mafia kilometa 52.16?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa majibu yako mazuri, nina maswali mawili ya nyongeza.

Je, ni lini barabara ya Mbinga – Litembo – Meyangayanga katika Jimbo la Mbinga Mjini itajengwa kwa kiwango cha lami?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, ni lini Serikali itaweka taa kwenye barabara ya kutoka Hazina kupitia UDOM mpaka kule Iyumbu kwa sababu ni barabara ambayo hata viongozi wanapita hasa usiku?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, barabara ya Mbinga – Litembo imeshafanyiwa upembuzi yakinifu na Serikali inaendelea kutafuta fedha ili iweze kuijenga kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, kuhusu uwekaji wa taa za Hazina kwenda UDOM, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge ambaye mara kadhaa amekuwa akiliongelea. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tumejibu kwamba tulishapata orodha ya maeneo yote ambayo yana uhitaji, lakini pia kama Wizara tutapeleka taa 200 ambazo mkoa husika utahusika kuona maeneo yapi ni muhimu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba eneo alilotaja la Hazina – UDOM litakuwa ni moja ya maeneo ambayo yatakwenda kuwekewa taa, ahsante.

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. HAWA M. CHAKOMA Aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kilindoni – Rasimkumbi - Mafia kilometa 52.16?

Supplementary Question 2

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Spika, nashukuru, kwa kuwa barabara pekee ya kuingilia Ukerewe ya Lugizi - Nansio mkandarasi wake ana zaidi ya mwaka mzima amesimama kufanya kazi kwa kutolipwa advance payment na sasa ina…

SPIKA: Mheshimiwa Waziri, tafuta kiti uketi. Mheshimiwa Mkundi.

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Spika, barabara ya Lugizi - Nansio ambayo mkandarasi wake amesimama zaidi ya mwaka mmoja kwa kutolipa advance payment na barabara hii imekuwa kero kubwa kila siku magari yanakwama na ndiyo barabara pekee ya kuelekea Ukerewe; nini kauli ya Serikali sasa kwa wananchi wa Ukerewe kuhusu barabara hii?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge pia kwamba tumeshapata maelekezo pia ya Waziri Mkuu alivyokwenda huko kwamba tuweze kutafuta fedha ili kumlipa mkandarasi ambayo kimsingi alishafanya kazi, kwa hiyo, tulishapeleka hati za malipo Hazina na tuna uhakika muda sio mrefu atalipwa ili aweze kuendelea na kazi kukamilisha hiyo kazi ambayo ameshaianza, ahsante.

Name

Dr. Christine Gabriel Ishengoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. HAWA M. CHAKOMA Aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kilindoni – Rasimkumbi - Mafia kilometa 52.16?

Supplementary Question 3

MHE. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Barabara ya Bigwa – Kisaki mkandarasi amesimama, haendelei na kazi na hiyo barabara ni muhimu sana kwa sababu ya uzalishaji wa watu wa Morogoro, je, ni lini barabara hii na mkandarasi ataanza kujenga hiyo Barabara ya Bigwa - Kisaki?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, ni kweli kwamba barabara hiyo mkandarasi alishasaini mkataba na kinachosubiriwa ili aanze kazi ni kulipwa fedha ya awali kwa maana ya malipo ya awali na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tunasubiria malipo kutoka Hazina ili mkandarasi huyo aweze kulipwa na kuanza kazi ya Barabara ya Bigwa – Kisaki, ahsante.