Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Tumaini Bryceson Magessa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Primary Question
MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza: - Je, Serikali ipo hatua gani kwenye ujenzi wa kipande cha barabara kutoka Katoro hadi Daraja la Nyikonga kwenye Barabara ya Katoro – Ushirombo?
Supplementary Question 1
MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali kuhusu barabara ya kutoka Ushirombo – Katoro, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, je, upembuzi yakinifu uliofanyika miaka kadhaa iliyopita bado unafaa kwenye ujenzi wa barabara hiyo?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Geita kwa maana ya Mpomvu – Nyarugusu – Bukoli – Irogi?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, kuhusu kama upembuzi yakinifu na usanifu wa kina utakuwa unafaa au laa, wataalam watakwenda uwandani wakati kipande hiki kitakapotakiwa kuanza kujengwa na kupitia upya ule usanifu na kama kutakuwa na marekebisho basi wataalam watafanya hayo marekebisho yatakayohitajika.
Mheshimiwa Spika, kuhusu Barabara ya Mtakuja – Nyarugusu – Bukoli – Kakola nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari mkandarasi alishapatikana na kinachosubiriwa sasa hivi ni kwamba mkataba huo upo kwa Mwanasheria Mkuu kwa ajili ya vetting, ahsante.
Name
Deodatus Philip Mwanyika
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Njombe Mjini
Primary Question
MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza: - Je, Serikali ipo hatua gani kwenye ujenzi wa kipande cha barabara kutoka Katoro hadi Daraja la Nyikonga kwenye Barabara ya Katoro – Ushirombo?
Supplementary Question 2
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, ahsante, barabara inayoanzia Ramadhan – Iyai inayounga Mkoa wa Njombe kupita Jimbo la Njombe, Halmashauri ya Mji wa Njombe – Wanging’ombe, ni lini barabara hii itapata fedha za kutosha ili ikamilishwe?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, Ramadhan – Iyai kilometa 74 imeshafanyiwa usanifu na kwa sasa tumekuwa tukiijenga kwa awamu na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika bajeti ya mwaka tunaouendea wa 2025/2026 tumeitengea fedha ili iweze kuanza kujengwa, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved