Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jonas William Mbunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Mjini

Primary Question

MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa maboma ya madarasa, nyumba za walimu na vyoo kwenye shule za msingi na sekondari Halmashauri ya Mbinga utakamilika?

Supplementary Question 1

MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kuishukuru Serikali kwa majibu yake mazuri, lakini nina maswali mawili. Swali la kwanza; pamoja na utekelezaji na ukamilishaji wa maboma, maboma yaliyokamilishwa kwa sehemu kubwa ni yale ya shule za msingi. Je, ni lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kukamilisha maboma ya shule za sekondari?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Serikali ilikuwa na mpango wa kuendelea kujenga maabara kwenye shule mbalimbali za Sekondari za Kata. Ni lini sasa Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kujenga maabara hizo kwenye shule za sekondari? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kukamilisha maboma ya madarasa katika shule za msingi na pia katika shule za sekondari. Katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga Serikali imeshapeleka fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge, ni kweli fedha nyingi zimetengwa kukamilisha maboma ya shule za msingi kwa sababu yalikuwa mengi zaidi na uhitaji wa madarasa ulikuwa mkubwa zaidi. Hata hivyo, katika bajeti ya kila mwaka Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kukamilisha maboma ya shule za msingi na sekondari. Vivyo hivyo katika Mwaka huu wa Fedha wa 2025/2026, Serikali imetenga bajeti hiyo. Kwa hiyo, napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunda kwamba maboma ya shule za sekondari katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga pia yamepangiwa fedha kwa ajili ya ukamilishaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kuhusu ujenzi wa maabara, Serikali hii ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya mapinduzi makubwa katika ujenzi wa maabara. Lengo likiwa ni kuhakikisha watoto wetu wanajifunza kwa vitendo masomo ya sayansi na maabara zimeendelea kujengwa. Katika Mwaka huu wa Fedha 2025/2026, ninamhakikishia Mbunge bajeti ya ujenzi wa maabara imetengwa na tutaendelea kujenga katika halmashauri hiyo na halmashauri zingine kote nchini. Ahsante sana.

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa maboma ya madarasa, nyumba za walimu na vyoo kwenye shule za msingi na sekondari Halmashauri ya Mbinga utakamilika?

Supplementary Question 2

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mheshimiwa Waziri, Shule ya Sekondari ya Ikuti katika Wilaya ya Rungwe ina upungufu katika mabweni ya wanafunzi hasa vijana. Ni lini Serikali itaongeza nguvu ili kuweza kusaidia mabweni hayo kujengwa? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Ni kweli kwamba tunahitaji kujenga mabweni katika shule zetu ikiwemo Shule ya Ikuti na tunafahamu Serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Shule ya Sekondari ya Ikuti imepangwa kujengewa mabweni. Serikali itahakikisha inapeleka fedha kwa ajili ya kujenga mabweni na kuboresha huduma za elimu kwa wanafunzi.