Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI aliuliza:- Je, Serikali imejipangaje kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambayo yanachangia uharibifu wa mazingira?
Supplementary Question 1
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali moja dogo la nyongeza lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na ushauri wangu kwa Serikali, kwamba Serikali iwahishe mchakato wa mipango kabambe ili kuweza kunusuru hali ya mabadiliko ya tabianchi iliyopo kwa sasa, ambayo ni hatarishi kabisa.
(a) Je ni kiasi gani Serikali imejipanga kutoa elimu kwa wananchi ili kunusuru hali ya hatari ya mabadiliko ya tabianchi inayoendelea sasa?
(b) Pamoja na mikakati mingine mingi mizuri ya Serikali je, Serikali ni kwa kiasi gani imejipanga kuhakikisha kwamba inatoa miche ya miti kwa Watanzania wote ili waweze kwenda kupanda na kuweza kukabiliana na hali ya mabadiliko ya tabianchi?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue fursa hii nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge, Mama Msongozi kwa kazi nzuri anayoifanya kwenye tasnia hii ya mazingira, hasa suala la mabadiliko ya tabianchi. Hivi karibuni nimemshuhudia katika vyombo vya habari akiwa anagawa mitungi ya gesi zaidi ya 2000. Pia nimeshuhudia akipanda miti, maana nami nilishiriki kule mkoani kwake kwenda kupanda miti. Nimpongeze sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mipango ya kutoa elimu ipo na ilishaanza na ipo endelevu, na hivi tunavyozungumza tunaendeleanayo. Tunao mpango wa kuendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya usimamizi wa vyanzo vya maji, hasa kwenye changamoto ya kuzingatia sheria ya mita 60. Hii imekuwa ni changamoto sana, kwa hiyo, tunaendelea kutoa elimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na suala la utunzaji wa taka na uhifadhi wa taka, kwa sababu bado imekuwa ni changamoto na bado wananchi wengi hawajafahamu kwamba taka ni fursa, tunayo jitihada ya kutoa elimu kuhusiana na suala la upandaji wa miti na masuala mengine ya kuishughulikia miti, kwa sababu watu wengi wamekuwa wanapanda miti, lakini kwenye kuishughulikia imekuwa ni changamoto.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, utunzaji wa fukwe na visiwa, kama mnavyojua, bado kuna changamoto ya bahari kuwa zinakula visiwa na hatimaye visiwa vile vinapotea. Kwa hiyo, tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kufahamu hilo. Huo ndiyo mpango tulionao katika elimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kutoa miti bure, ni kweli kwamba tumekuwa tukiuza baadhi ya miti kupitia taasisi inayosimamia miti, ingawa kuna baadhi ya miti ambayo ni ya kimkakati, huwa ni miti ambayo inatolewa bure.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba kutoa wito kwa taasisi zote au watu binafsi ambao wanatengeneza vitalu kwa ajili ya miti ya kupanda, basi watafute namna ambavyo wanaweza wakawasaidia wananchi kuweza kupata miti bure kwa kuwa huwa inauzwa ili kushughulikia gharama za uendeshaji, nakushukuru.
Name
Fatma Hassan Toufiq
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI aliuliza:- Je, Serikali imejipangaje kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambayo yanachangia uharibifu wa mazingira?
Supplementary Question 2
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza: -
Je, Serikali ina kauli gani kuhusiana na kuwashirikisha wanawake, hasa wale wa pembezoni katika kuandaa mipango na mikakati ya kukabiliana na tabianchi?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya miongoni mwa jambo ambalo Serikali haimwachi mtu yeyote, ni suala la kupambana dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa tumegundua kama Serikali kwamba miongoni mwa watu ambao ni waathirika wakubwa wa athari ya mabadiliko ya tabianchi ni wanawake na watoto, ndiyo maana Mama Samia Suluhu Hassan akaja na mkakati na sera ya masuala ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kumnusuru mama na binti na mambo mengine ya kimazingira, nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved