Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Flatei Gregory Massay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. FLATEI G. MASSAY K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka Gari la Wagonjwa kwenye Kituo cha Afya cha Mgori Jimbo la Singida Kaskazini?
Supplementary Question 1
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; je, pamoja na magari haya mawili uliyoyasema, Serikali ina mpango gani wa kuongeza gari moja katika ile Wilaya ya Singida kama swali la Mheshimiwa Mbunge linavyosema? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa Jimbo la Mbulu Vijijini ni kubwa na lina maeneo mengi ambayo hata Wahadzabe hawafikiki kwa magari. Je, ni lini watapeleka gari la wagonjwa katika maeneo haya niliyoyasema? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu hoja ya Mheshimiwa Mbunge ilikuwa ni gari la wagonjwa kwenye Kituo cha Afya cha Mgori na tayari Serikali imeshapeleka gari hilo katika hicho kituo cha afya cha Mgori, nimhakikishie tu kwamba, tunafahamu bado kuna uhitaji wa magari ya wagonjwa na Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya kupeleka hayo magari katika vituo ambavyo vina uhitaji mkubwa zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kuhusiana na kata na vituo vingine, Serikali imeweka mpango madhubuti wa kufanya kwanza tathmini ya mahitaji na umbali kutoka kituo kimoja kwenda kingine, ili kuhakikisha wakati tunanunua magari ya wagonjwa tunatoa kipaumbele zaidi kwenye kata au vituo vya afya vyenye idadi kubwa zaidi ya wananchi ambavyo vina umbali mkubwa zaidi kutoka hospitali ya halmashauri. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwamba Serikali itafanyia kazi hoja hizo zote mbili. Ahsante sana.
Name
Mussa Ramadhani Sima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Mjini
Primary Question
MHE. FLATEI G. MASSAY K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka Gari la Wagonjwa kwenye Kituo cha Afya cha Mgori Jimbo la Singida Kaskazini?
Supplementary Question 2
MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa tuna Kituo cha Afya cha Mtisi ambacho kiko mbali zaidi ya kilometa 20. Ni lini Serikali itapeleka gari la wagonjwa ili kuwasaidia wananchi wa Kata ya Mtamaa? Ninakushukuru.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya cha Mtisi ambacho kiko umbali wa zaidi ya kilometa 20, tutakwenda kufanya tathmini pia kuona idadi ya wananchi wanaotibiwa katika eneo hilo. Pia, tutaenda kuhakikisha kwamba tunatenga bajeti kwa ajili ya kununua magari ya wagonjwa kwa ajili ya kupeleka katika vituo vyote vya afya ambavyo vina uhitaji mkubwa kikiwemo kituo hiki ambacho Mheshimiwa Mbunge amekitaja. Ahsante.
Name
Kunti Yusuph Majala
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FLATEI G. MASSAY K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka Gari la Wagonjwa kwenye Kituo cha Afya cha Mgori Jimbo la Singida Kaskazini?
Supplementary Question 3
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya cha Farkwa ni kipya, tunaishukuru Serikali kwa kutusogezea hiyo huduma kwa wananchi wetu lakini hatuna gari la wagonjwa. Nini mkakati wa Serikali kupeleka gari la wagonjwa kwenye Kituo cha Afya cha Farkwa? Ninakushukuru.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, bahati nzuri tumefanya ziara na Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum na Mbunge wa Jimbo pale Farkwa mwezi mmoja uliopita. Tuliona kweli inahudumia wananchi walio wengi, lakini pia kuna uhitaji wa gari la wagonjwa. Ninaomba nimhakikishie Mbunge kwamba tumeshakiweka Kituo cha Afya cha Farkwa kwenye mpango wa magari yatakayofuata awamu hii kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanapata gari la wagonjwa ili kuboresha huduma za dharura na huduma za rufaa. Ahsante.
Name
Benaya Liuka Kapinga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbinga Vijijini
Primary Question
MHE. FLATEI G. MASSAY K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka Gari la Wagonjwa kwenye Kituo cha Afya cha Mgori Jimbo la Singida Kaskazini?
Supplementary Question 4
MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya Litumbandyosi, Kituo cha Afya Matiri na Kituo cha Afya cha Mkumbi pamoja na Hospitali ya Halmashauri hawana gari la wagonjwa. Ni lini sasa tutapeleka gari la wagonjwa katika maeneo hayo? Ahsante sana.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Kapinga amefuatilia mara kadhaa na tayari kwenye mpango wa magari ya wagonjwa unaofuata kupitia Wizara ya Afya, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambalo ni Jimbo la Mbinga Vijijini tayari limeshawekewa gari moja kwa ajili ya Hospitali ya Halmashauri.
Name
Dr. Charles Stephen Kimei
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vunjo
Primary Question
MHE. FLATEI G. MASSAY K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka Gari la Wagonjwa kwenye Kituo cha Afya cha Mgori Jimbo la Singida Kaskazini?
Supplementary Question 5
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Vunjo lenye wakazi 260,000 lina gari moja tu la kubeba wagonjwa. Je, ni lini watatupatia magari kwenye vituo vya Magarubu Headquarters, Kirua Vunjo Magharibi na Kahe Magharibi? Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Jimbo la Vunjo lina gari moja la wagonjwa na kwa kweli katika eneo ambalo tumelipa kipaumbele cha hali ya juu katika majimbo ni Jimbo la Vunjo. Nimhakikishie Mheshimiwa Dkt. Kimei kwamba, kwenye mgao unaofuata wa magari ya wagonjwa kupitia Wizara ya Afya tayari tumesha-allocate gari moja la wagonjwa kwa ajili ya Jimbo la Vunjo. (Makofi)
Name
Shabani Omari Shekilindi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lushoto
Primary Question
MHE. FLATEI G. MASSAY K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itapeleka Gari la Wagonjwa kwenye Kituo cha Afya cha Mgori Jimbo la Singida Kaskazini?
Supplementary Question 6
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilituahidi gari la wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto. Je, ni lini gari hilo litapelekwa? Ninakushukuru. (Makofi)
Name
Dr. Elly Marko Macha
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, tutaendelea kutenga fedha katika kila bajeti ya mwaka kwa ajili ya kupeleka magari ya wagonjwa kwenye hospitali za halmashauri na vituo vya afya vyenye uhitaji mkubwa wa magari ya wagonjwa. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Shekilindi kwamba, Hospitali ya Halmashauri ya Lushoto ni moja ya Hospitali ambazo zitaingizwa kwenye mpango na fedha itatafutwa kwa ajili ya kupeleka gari la wagonjwa.