Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Venant Daud Protas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Igalula
Primary Question
MHE. VENANT D. PROTAS K.n.y. MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: - Je, lini Serikali itamaliza kusambaza umeme kwenye vitongoji vyote nchini?
Supplementary Question 1
MHE. VENANT D. PROTAS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwanza naipongeza Wizara na Serikali kwa hatua kubwa ya vitongoji zaidi ya 30,000 kuwa vimefikiwa umeme.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu dogo la nyongeza ni kwamba, kwenye bajeti hii ambayo tunaendelea nayo, walituahidi Wabunge kila jimbo mtatupatia vitongoji 15 ikiwemo Jimbo la Igalula ambako tulipeleka orodha kila Mbunge vitongoji 15. Jimbo la Igalula tulipeleka kwenye vitongoji vya Nyapimbi, Makungu na kwenye maeneo mengine. Mpaka leo tunakwenda kumalizia ngwe ya bajeti hii, hakuna mkandarasi aliyanza ujenzi wa vitongoji hivyo 15. Je, Serikali ina kauli gani kwa wakandarasi ambao wameshawapa mkataba na bado hawajaingia site?
Name
Judith Salvio Kapinga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Mbunge. Katika miradi hii ya vitongoji 15 katika mikoa yote, tayari tumeshapata wakandarasi; na kwa kweli katika mikoa mingi wakandarasi wako site, walikuwa wanatafuta vifaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye baadhi ya mikoa tayari vitongoji hivi vimeshaanza kazi na baadhi, vifaa ndiyo vinakwenda. Kwa upande wa Igalula tutafuatilia kama kuna changamoto yoyote, na baada ya hapo tutaendelea kumsimamia mkandarasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto tuliyonayo ni kwamba, wakandarasi hawa wanafanya kazi katika majimbo yote kwenye mkoa. Kwa hiyo, issue inakuja pale kwenye kuanza kwenye jimbo moja baada ya nyingine, kwa sababu mkandarasi ana scope maalum ya utekelezaji wa mradi. Kulingana na muda, naomba Waheshimiwa Wabunge tuwape muda, wakandarasi wengi wako site, wana uwezo, na watawafikia kwenye maeneo yenu, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved