Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tumaini Bryceson Magessa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Primary Question

MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza: - Je, ujenzi wa Barabara ya Mpomvu kupitia Nyarugusu kwenda Bulyankulu kwa kiwango cha lami upo katika hatua gani?

Supplementary Question 1

MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri Mheshimiwa Waziri yanayotia matumaini kwamba wako kwenye hatua za mwisho, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la kwanza: ni lini barabara ya kutoka Ushirombo kuja Katoro itajengwa kwa lami kwa sababu iko kwenye bajeti hususan kipande kile cha kutoka Nyikonga kuja Katoro? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, je, Waziri yuko tayari kuambatana nami kwenda Jimboni ili akazione barabara hizi na ajue, kwa nini tunaendelea kuzisema kila mwaka, kwa sababu zina uhitaji wa wananchi? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na swali la pili, niko tayari kutembelea hizi barabara, na bahati nzuri hizi barabara ninazifahamu kwa sababu nimeshazitembelea. Kwa hiyo, kwa ajili ya kwenda na Mheshimiwa Mbunge kukutana na wananchi, niko tayari tutakapokuwa tumepata ratiba nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu barabara ya Ushirombo kwenda Katoro, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tumeshaanza kazi. Tumeanza na kilometa 5.3 kutoka Ushirombo hadi sehemu inayoitwa Bwenda, na mkandarasi ameshapatikana yuko kwenye hatua za awali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, kutoka Kashelo kwenda kwenye Daraja la Nyikonga pamoja na daraja lake, tunajenga kwa Mpango wa World Bank kupitia Mpango wa Rais na hivi sasa tuko hatua za manunuzi na eneo ambalo tutajenga hapo kama kilometa 10.4. Kwa hiyo, maeneo yaliyobaki, Serikali inaendelea kutafuta fedha kukamilisha barabara yote yenye urefu wa kilometa kama 58. (Makofi)