Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Stephen Lujwahuka Byabato
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Mjini
Primary Question
MHE. STEPHEN L. BYABATO aliuliza:- Je, kwa nini watumishi wanaojitolea wanapoajiriwa wasipangiwe katika Vituo walivyokuwa wakijitolea kama kipaumbele cha kwanza?
Supplementary Question 1
MHE. STEPHEN L. BYABATO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali lakini nina swali moja la nyongeza. Kwanza ninampongeza sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza mishahara ya watumishi na kuwafanya wawe na morali na hamu ya kuendelea kufanya kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo Wabunge wenzangu wameuliza kwenye maswali mengi ya TAMISEMI, ninapenda kufahamu ni upi hasa mkakati wa Serikali wa kuhakikisha inapunguza ma-gap ya ajira ambayo yapo kwenye ikama za Utumishi wa Umma dhidi ya ile ambayo inapatikana kwa sasa. Ni upi mkakati wa Serikali ambao utaondoa kabisa tatizo hili la upungufu wa Watumishi wa Umma? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Byabato kwa kazi nzuri anazozifanya za uwakilishi wa wananchi wake wa Jimbo la Bukoba Mjini.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikijibu swali lake la jumla; jitihada za Serikali katika kipindi hiki cha Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ajira mpya zilizokuwa zimejazwa ni takribani ajira 149,000, lakini ajira mbadala ambazo Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alizitolea kibali ni 39,963. Pia, hivi juzi katika jitihada ileile, Mheshimiwa Rais ametoa kibali cha ajira nyingine ambazo zinatakiwa zijazwe kabla ya kwisha kwa mwaka huu wa fedha, ajira 33,212. Hii yote ni jitihada na hata hivyo katika bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora tayari kuna ikama imetengwa kwa ajili ya ajira mpya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali ina mpango wa dhati na tutaendelea kujaza mapungufu ya ukosefu wa watumishi kadri ya upatikanaji wa fedha. (Makofi)
Name
Janejelly Ntate James
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. STEPHEN L. BYABATO aliuliza:- Je, kwa nini watumishi wanaojitolea wanapoajiriwa wasipangiwe katika Vituo walivyokuwa wakijitolea kama kipaumbele cha kwanza?
Supplementary Question 2
MHE. JANEJELLY J. NTATE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niipongeze Serikali kwa kutupatia kicheko, furaha na amani watumishi wa Tanzania. Swali langu la nyongeza na nilishauliza mara nyingine hapa; ni lini sasa Serikali itaweka rasmi kigezo cha kujitolea kama sifa ya mtumishi kuajiriwa? (Makofi)
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, niendelee tena kumpongeza Mheshimiwa Kamishna Janejelly kwa namna anavyofuatilia masuala ya watumishi. Kama nilivyokwisha kujibu hapa Bungeni ni kwamba tayari tumeandaa mwongozo wa wale wanaojitolea ambao tunaanza kuutumia rasmi tarehe Mosi Julai, mwaka huu. Ndani ya mwongozo huo tumeelekeza namna ambavyo kwanza wanaojitolea watapewa fedha ya kujikimu na namna ambavyo tutaweza kuwapa kipaumbele pale ajira zinavyotangazwa. Ninakushukuru sana. (Makofi)
Name
Issaay Zacharia Paulo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Primary Question
MHE. STEPHEN L. BYABATO aliuliza:- Je, kwa nini watumishi wanaojitolea wanapoajiriwa wasipangiwe katika Vituo walivyokuwa wakijitolea kama kipaumbele cha kwanza?
Supplementary Question 3
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, kwa kuwa tatizo la ukosefu wa walimu wa sayansi nchini limekuwa kubwa sana. Je, ni kwa nini Serikali isione utaratibu wa mfumo rasmi au mfumo maalum wa kuajiri walimu wa sayansi katika shule zetu ili kuondoa tatizo hilo? Ninakushukuru sana.
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwamba Mheshimiwa Rais ametoa kibali cha ajira 33,212 ambazo zinatakiwa kujazwa kabla ya kukamilika kwa mwaka huu wa fedha. Kati ya hizo ajira, zipo ajira 9,000 ambazo zinaenda kwenye kada ya walimu na wengi waliopo asilimia kubwa ni walimu wa masomo ya sayansi. Kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, katika ajira hizi vijana wengi wataarijiwa wa masomo ya sayansi ili kuziba gap hilo la upungufu wa walimu wa sayansi.
Name
Jesca Jonathani Msambatavangu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Primary Question
MHE. STEPHEN L. BYABATO aliuliza:- Je, kwa nini watumishi wanaojitolea wanapoajiriwa wasipangiwe katika Vituo walivyokuwa wakijitolea kama kipaumbele cha kwanza?
Supplementary Question 4
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, Manispaa ya Iringa tulipewa kibali cha kuajiri watendaji 23, lakini baadaye tukaambiwa tusubiri barua ya Katibu Mkuu. Sasa ninaomba kujua ni lini barua hiyo itatoka na wewe kama Naibu Waziri utusaidie ili wale watoto waajiriwe? Ninakushukuru.
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, Nikijibu swali la Mheshimiwa Jesca nitaomba baada ya kumaliza kipindi cha maswali na majibu tukae tufuatilie jambo hilo ili tuone. Ni kweli tulisitisha kupisha zoezi la kuajiri walimu na baadaye sasa tumeendelea na taratibu za kuendelea na ajira nyingine. Kwa hiyo tutakutana pamoja tuone limeishia wapi, kama ni jambo ambalo limekwama, basi tutamaliza ili muweze kuendelea na utaratibu huo. Ninakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved