Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Vita Rashid Kawawa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Namtumbo
Primary Question
MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: - Je, kwa nini ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma umesimama?
Supplementary Question 1
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa kuwa katikati hapo mradi huu ulisimama na ukawa unatutia shaka na sisi tulikuwa tunataka huduma kwenye hospitali hiyo ya rufaa kwa sababu watu wanakwenda mpaka Mbeya au Dar es Salaam. Ni lini sasa Serikali itaharakisha ujenzi wa hospitali hiyo kwa awamu hizo zilizobakia ili tuweze kupata huduma pale pale Mkoa wa Ruvuma? (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji huo, lakini kama ambavyo anajua, wana hospitali ambayo ina uwezo na ukubwa kama hospitali ya mkoa, lakini hospitali anayoizungumzia ni hospitali inayojengwa kwenye eneo jipya ili baadaye kuachia hii ambayo ipo sasa kuwa ni hospitali ya Wilaya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imejenga katika awamu hizi tatu. Kabla ya mwisho wa mwaka wa bajeti ya 2025/2026, tutakuwa tumefika awamu ya pili, na itakuwa imebaki kazi ndogo sana ili kuweza kukamilisha. (Makofi)
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: - Je, kwa nini ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma umesimama?
Supplementary Question 2
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mpango gani wa kutuletea CT-Scan katika Hospitali ya Wilaya ya Hai ambayo inahudumia pia wananchi kutoka Wilaya ya Siha? (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kuijali hospitali yake ya wilaya, lakini nimkumbushe tu kwamba hospitali yetu ya Mkoa wa Kilimanjaro (Mawenzi) tayari imesimikwa CT-Scan.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama unavyojua, unaposimika CT-Scan ni miundombinu, lakini hasa hasa siyo miundombinu, ni utaalamu. Yaani kwa maana ya madaktari wabobezi na kwa maana ya hospitali ya level ya wilaya, bado mkakati huo haujaanza kwa maana ya kutengeneza miundombinu, na pia kuweka wataalamu wenye uwezo wa kusimamia mashine hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa sasa kwa wilaya yetu ya Siha na Wilaya yake kwa kutumia Hospitali ya Mawenzi na hata Hospitali ya Kibongoto ambayo ni kilometa chache kutoka kwenye Jimbo lake, mambo yataendelea kuwa mazuri kwa watu wa Hai.
Name
Regina Ndege Qwaray
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: - Je, kwa nini ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma umesimama?
Supplementary Question 3
MHE. REGINA N. QWARAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Hospitali yetu ya Mkoa wa Manyara haina kabisa wodi kwa ajili ya wagonjwa wanaume na kwa ajili ya wagonjwa wanawake. Je, ni lini Serikali itakwenda kujenga wodi hizo ili huduma ziendelee kutolewa? (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Mkoa wa Manyara ni hospitali ambayo kwa sasa, kwa kweli inafanya huduma kama Hospitali ya Mkoa. Hospitali ya Mkoa wa Manyara ilianza kama hospitali ikitumia jengo la mama na mtoto kama ndiyo sehemu ya OPD. Kwa hiyo, najua anachosema ni kwenye kuongeza wodi ya akina baba, lakini na wodi ya akina mama. Katika awamu hii, bajeti hii ya mwaka huu imetengwa shilingi bilioni tatu kwa ajili ya kutazama kwenye huo mkoa wake kuona ni nini ambacho kina kasoro ili kiweze kujengwa.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved