Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jesca Jonathani Msambatavangu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Primary Question

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza:- Je, lini NHIF itajumuisha huduma za afya ya akili kwenye vifurushi vya bima ya afya?

Supplementary Question 1

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru, lakini nina maswali mawili ya nyongeza baada ya majibu hayo. Swali la kwanza; Mheshimiwa Naibu Waziri aliahidi hapa kwamba mwezi huu Mei, Baraza la Afya ya Akili litakuwa limeanzishwa nchini. Je, limeshaanzishwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Mheshimiwa Naibu Waziri ni daktari, anadhani ni sawa watu wanaotaka kujinyonga kufungwa au kupelekwa hospitali? Ahsante.

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze dada yangu ambaye ni mtu wetu mzuri sana katika kupigania matatizo ya afya ya akili.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama ambavyo amesema kwenye swali lake la kwanza, tulikubaliana hapa Bungeni kwani aliuliza swali na tukakubaliana kufika wakati huu tutajitahidi ili kuweza kuanzisha hili baraza na kwa kweli mchakato bado unaendelea. Tumwombe tu atupe muda, kwa sababu kuna mambo ya muhimu ya kuzingatia kabla ya kuanzisha hilo ili kuweza pia kuyatafakari kwa kina yaliyojitokeza kwenye swali lake la pili, ili wakati tunaenda kuanzisha basi tuwe na miongozo mizuri ambayo itaweza kutufikisha tunapotaka kwenda.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, kusema ukweli wakati mwingine ni kazi kubwa sana ya kitaalam inahitajika kuweza kujua anayefanya hili ni amefanya kwa makusudi au amefanya kwa sababu ana matatizo ya akili na inahitajika kufanya uchunguzi wa kisayansi ili kuweza kuthibitisha na kuamua sasa mwelekeo ni upi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana ukienda Mirembe utakuta kabisa kuna hawa waliofanya matendo kama hayo kweli ni wafungwa, lakini wako Mirembe wakiendelea kutibiwa na wakihudumiwa na Serikali moja kwa moja wala bila kuhusisha familia zao. Kwa hiyo ninachoweza kukisema, hebu iachie vyombo (vyombo vya ulinzi na wataalamu wa tiba) waweze kuamua hayo yote na sisi tuamini kabisa wanapoamua wanaamua kwa usahihi.