Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Angelina Adam Malembeka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kurejesha kilimo cha pamba katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania?

Supplementary Question 1

MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya ziada. Kwanza namshukuru sana Naibu Waziri kwa majibu yake yaliyohusisha karantini ya mwaka 1947 ambapo ni miaka 51 iliyopita na kuhuishwa tena mwaka 2000, miaka 25 iliyopita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maswali yangu ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, tuna vyuo vya kilimo ikiwemo Chuo Kikuu cha SUA, Morogoro; tuna Uyole, Mbeya; tuna Ukiruguru, Mwanza; Tengeru, Arusha; Naliendele, Mtwara; na vinginevyo. Kule tuna wataalamu wa kutosha na watafiti makini. Je, ndani ya miaka hiyo 51 hadi sasa wameshindwa kufanya utafiti na kupata suluhisho la kuondoa funza mwekundu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili. Ndani ya miaka hiyo 51 baada ya utafiti wa awali, kilimo cha mwaka 1947 ni tofauti na kilimo cha miaka hii ya 2020. Tuna tofauti kuanzia kwenye pembejeo za kilimo, vifaa, dawa, mbegu na hata usimamizi. Je, Serikali imejipangaje kuondoa tatizo hili ili zao la pamba lilimwe tena katika mikoa ya Kusini? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nami nampongeza sana Mheshimiwa Malembeka kwa kazi nzuri ya kufuatilia kurejeshwa kwa zao la pamba katika mikoa ya Kusini. Nimthibitishie jambo moja kwamba, tafiti ni sayansi na sayansi inachukua hatua, ni mchakato (process). Kwa hiyo, hatuwezi tukatoa matamko ya kisiasa kulazimisha vyuo vikuu ama taasisi zilizo chini yetu kwa mfano, hizo TARI alizozieleza kwamba jamani mwakani muwe mmemaliza tafiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, sisi jukumu letu ni kuhakikisha kwamba wanaendelea kutafuta teknolojia bora na ya kisasa, lakini vilevile, wanaendelea kufanya tafiti kwa kadiri ya utaratibu ambao wamejiwekea. Kwa hiyo, sisi kama Wizara ya Kilimo tunatambua kwamba Chuo Kikuu cha SUA pamoja na Taasisi zetu za tafiti nchini bado wanaendelea na tafiti, na zitakapokamilika maana yake watatoa majibu na kukabiliana na huyu funza mwekundu ili tuweze kurejesha kilimo cha pamba katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwondoe tu shaka Mheshimiwa Mbunge kwamba kazi bado inaendelea, na utafiti kwa sababu ni sayansi, tuwaache wanasayansi waendelee kufanya hiyo kazi. (Makofi)

Name

Oran Manase Njeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbeya Vijijini

Primary Question

MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kurejesha kilimo cha pamba katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania?

Supplementary Question 2

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa je, ni lini huo utafiti utakamilika ili wananchi wa vijiji vya Kata za Mjele na Kata za Ikukwa Wilaya ya Mbeya waweze kurudi na kulima pamba ili nao waweze kupata mapato kiuchumi? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kama ambavyo nilijibu katika swali la nyongeza la mwuliza swali kwamba utafiti ni mchakato, tafiti ni sayansi na tafiti siyo masuala ya kutoa matamko. Kwa hiyo, siwezi kusema lini utafiti utakamilika. Tuwaache wanasayansi waendelee kufanya utafiti na shughuli hii itakapokamilika watatupa taarifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, wapo katika hatua nzuri kwa sababu muda wote wako site kuhakikisha kwamba wanakabiliana na huyu funza mwekundu. Kwa hiyo, ninaamini kulingana na mabadiliko ya teknolojia, mwafaka utapatikana mapema iwezekavyo. (Makofi)

Name

Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kurejesha kilimo cha pamba katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania?

Supplementary Question 3

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba zao la pareto linalimwa kwa ufanisi mkubwa hasa katika Mkoa wa Iringa Wilaya ya Kilolo, Wilaya ya Mufundi na Wilaya ya Iringa yenyewe? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Moja ya zao ambalo sisi kama Serikali tunalipa kipaumbele sasa hivi ni pamoja na zao la pareto, na nchi yetu sasa hivi ni ya pili kwa uzalishaji wa pareto Afrika, nafikiri na duniani. Kwa hiyo, jukumu letu ni kuongeza kasi kwa kutoa elimu kwa wakulima ili waweze kuingia katika kilimo cha pareto hususan katika maeneo ambayo umeainisha kama Kilolo, Mufindi pamoja na Iringa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaendelea kufanya hivyo kwa kutumia Maafisa Ugani na vyombo vya habari kuhabarisha umma juu ya umuhimu wa wakulima kuingia katika kilimo cha pareto. (Makofi)

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kurejesha kilimo cha pamba katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania?

Supplementary Question 4

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naishukuru Serikali, imeshafanya utafiti Jimbo la Mbulu Vijijini kwamba linafaa kulima zao la vitunguu swaumu. Je, ni lini sasa wanapeleka fedha kujenga mabwawa yote ambayo tumekubaliana na ipo kwenye bajeti ya mwaka huu?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, natambua kwamba Mheshimiwa Flatei Massay anafahamu kwamba utaratibu wa bajeti katika nchi yetu ni cash budget, na kwa sababu tunatumia mfumo huo, ni kwamba sisi tunavyopewa fedha, tunazigawanya kwenda katika maeneo yote nchini ikiwemo katika Jimbo lake la Mbulu Vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tutaendelea kuleta fedha kuhakikisha mabwawa yote ambayo tumeyaainisha katika Jimbo la Mbulu Vijijini yanakamilika kwa wakati kulingana na jinsi ambavyo tumeyaweka katika mipango yetu. (Makofi)