Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mustafa Mwinyikondo Rajab
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Dimani
Primary Question
MHE. MUSTAFA MWINYIKONDO RAJAB aliuliza:- Je, Idara ya Uhamiaji ina mpango gani wa kujenga hospitali Zanzibar kama ilivyo kwa Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama?
Supplementary Question 1
MHE. MUSTAFA MWINYIKONDO RAJAB: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina masuali mawili ya nyongeza. Kwanza ninaipongeza Idara yetu ya Uhamiaji kwa kuwa na majengo mazuri na ya kisasa kwa upande wa Zanzibar. Swali langu la kwanza; ni lini sasa mpango huu utaanza?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; kwa kuwa tunaanzisha zahanati naamini kwamba kutahitajika wataalam wa kada za afya. Je, Idara ya Uhamiaji ina mpango gani kuwapata wataalam hawa kwa kipindi hiki?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mustafa Mwinyikondo Rajab, Mheshimiwa Mbunge wa Diwani kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu la msingi ni kwamba, mara baada ya kupokea mwongozo kutoka Wizara ya Afya Zanzibar ndipo tutakapoanza ujenzi mara moja wa zahanati hii ya kuhudumia Askari pamoja na wananchi wanayoizunguka.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili kuhusu wataalam, wataalam wapo, lakini Idara pia itaendelea kuajiri hatua kwa hatua kuhakikisha kwamba inakidhi mahitaji ya kutoa huduma katika zahanati ambayo itajengwa. Ahsante sana.
Name
Edward Olelekaita Kisau
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kiteto
Primary Question
MHE. MUSTAFA MWINYIKONDO RAJAB aliuliza:- Je, Idara ya Uhamiaji ina mpango gani wa kujenga hospitali Zanzibar kama ilivyo kwa Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama?
Supplementary Question 2
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti ya Serikali 2024/2025, iliweka pesa kwa ajili ya vituo vya Polisi vilivyoanzishwa na wananchi vya Magungu – Lengatei – Matui na Chekanao. Je, ni lini pesa hizi zitakwenda?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Edward Olelekaita, Mbunge wa Kiteto kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli katika Mwaka huu wa Fedha 2024/2025, vimetengwa vituo vya Polisi kwa Jimbo la Kiteto kama alivyovitaja karibu vituo vinne na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba bado mwaka wa fedha haujakwisha, Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Polisi kama alivyosema. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved