Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Florence George Samizi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Primary Question

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza:- Je, lini Serikali itakarabati Skimu za Umwagiliaji za Nyendara, Muhambwe, Kumbanga, Mgondogondo na Kigina, Muhambwe?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi. Kwanza nishukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, hata hivyo ninayo maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa, Serikali imethibitisha kwamba, Juni, Mwaka 2025 upembuzi yakinifu utaisha. Nini commitment ya Serikali kutenga pesa ya kujenga na kukarabati skimu hizi kwenye bajeti ya mwaka 2025/2026?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; Skimu hizi za Jimbo la Muhambwe zina ukubwa wa hekta 1,297 na kati ya hizi ni hekta 582 tu zinazofanya kazi kwa maana ya kulimwa, chini ya 50%. Je, Serikali haioni kwamba, iko sababu ya kuharakisha kutengeneza hizi skimu ili wakulima wa Jimbo la Muhambwe waweze kufaidika na skimu hizi?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Dkt. Samizi Florence kwa kazi nzuri anayoifanya kwa Wananchi wake wa Jimbo la Muhambwe, hususan kufuatilia hii miradi. Jambo moja ambalo nimhakikishie ni kwamba, miradi hii yote ambayo upembuzi yakinifu umekamilika tumeitengea fedha katika Mwaka wa Fedha unaokuja 2025/2026. Kwa hiyo, baada ya hii maana yake ni inaingia katika Mwaka unaokuja, tutazitangaza na zitaanza kufanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kuongeza ukubwa, ili kufanya haraka, ni kwamba, tunatambua kwa sasa ukubwa ni hekta 582 na huu usanifu wa kina umekusudia kuongeza eneo la umwagiliaji kufikia hizo hekta 1300 kwa hiyo, lipo katika mipango ambayo tunayo. Nimthibitishie tu tutakapozitangaza, tutatangaza katika ukubwa ambao upo kwa sasa. Ahsante.

Name

Sylivia Francis Sigula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza:- Je, lini Serikali itakarabati Skimu za Umwagiliaji za Nyendara, Muhambwe, Kumbanga, Mgondogondo na Kigina, Muhambwe?

Supplementary Question 2

MHE. SYLIVIA F. SIGULA: Mheshimiwa Naibu Spika, Skimu ya Umwagiliaji iliyoko Ilemba, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, kasi ya ujenzi hairidhishi kabisa. Mkataba ulipaswa kukamilika mwaka jana, Disemba, 2024 wameongezewa mwaka mzima, lakini bado kasi hairidhishi. Je, uko tayari kufika site kuona namna ambavyo kasi hairidhishi, ili utoe maelekezo kwa mkandarasi huyo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, niko tayari kufika site na yeye pamoja na Mbunge wa jimbo. Nimthibitishie tu kwamba, tumepata fedha na tutapeleka ili yule mkandarasi amalizie kazi. Ahsante.

Name

George Natany Malima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza:- Je, lini Serikali itakarabati Skimu za Umwagiliaji za Nyendara, Muhambwe, Kumbanga, Mgondogondo na Kigina, Muhambwe?

Supplementary Question 3

MHE. GEORGE N. MALIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa Bwawa la Msagali unaenda kwa kusuasua sana. Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Bwawa la Umwagiliajai la Msagali?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, Bwawa la Msagali ambalo lipo katika Jimbo la Mpwawa liko katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Bahati nzuri eneo hilo nimefika, kusuasua kwake ni kwamba, sisi tulikuwa tumechelewesha kupeleka fedha ambazo tulikuwa bado hatujazipata, lakini katika mgao huu ambao tumeupata, kwa mwezi ujao, tutaongeza zile fedha, ili mkandarasi aweze kumaliza ile kazi iliyobakia. Ahsante.

Name

Martha Festo Mariki

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza:- Je, lini Serikali itakarabati Skimu za Umwagiliaji za Nyendara, Muhambwe, Kumbanga, Mgondogondo na Kigina, Muhambwe?

Supplementary Question 4

MHE. MARTHA F. MARIKI: Mheshimiwa Naibu Spika, Ujenzi wa Skimu za Umwagiliaji za Mwamkulu, Ugawa pamoja na Uwila umekuwa ukisuasua na Serikali imeshatenga fedha nyingi sana, lakini hazijakamilika. Je, upi mpango wa Serikali wa kutenga fedha kukamilisha ujenzi huo, ili kuleta tija kwa wananchi? Ninakushukuru.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwamba, mabwawa yote matatu aliyoyaainisha Mheshimiwa Mbunge tumeyatengea fedha na sisi tumekuwa tukitoa fedha kulingana na tunavyopokea kutoka Wizara ya Fedha. Kwa hiyo, tutaendelea kupeleka fedha ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati. Ahsante.

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza:- Je, lini Serikali itakarabati Skimu za Umwagiliaji za Nyendara, Muhambwe, Kumbanga, Mgondogondo na Kigina, Muhambwe?

Supplementary Question 5

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Naibu Spika, Skimu ya Umwagiliaji ya Ruaha Mbuyuni, vifaa vimewekwa pale na mkandarasi, sasa ni miezi miwili, lakini kazi haianzi. Je, ni lini mkandarasi yule ataanza kazi kujenga ile skimu ambayo ilibomoka? Ninakushukuru.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwamba, tulishamkabidhi mkandarasi site katika Jimbo la Kilolo, alichotakiwa kukifanya sasa hivi ni kwamba, aanze kazi na sisi kama Serikali tulishamlipa advance payment kwa kazi hiyo. Kwa hiyo, niseme tu kwamba, mimi mwenyewe nitafuatilia kwa kuwaelekeza watu wa RM wa Mkoa wa Iringa, ili ahakikishe anamsukuma mkandarasi aanze ile kazi mara moja. Ahsante sana.