Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ally Juma Makoa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kondoa Mjini
Primary Question
MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la zimamoto Wilaya ya Kondoa ili kukabiliana na majanga ya moto yanayotokea mara kwa mara?
Supplementary Question 1
MHE. ALLY J. MAKOA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu ya Serikali. Nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa majanga ya moto yameendelea kuharibu mali za wananchi, ni lini Serikali inatuahidi kutuletea haya magari ili kuwapa matumaini hawa wananchi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; ili kuyatunza magari haya, nini mpango wa Serikali kuhakikisha maeneo yote yaliyotajwa yatafikiwa na gari hizi zitapata parking bora kwa ajili ya kuyahifadhi?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Ally Juma Makoa kwamba, mradi huo tayari umeshatekelezwa na magari yameshanunuliwa, na awamu ya kwanza tayari yameshaingia hapa nchini. Awamu ya pili itaingia mwezi Agosti, 2025. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba gari litafika katika Halmashauri ya Kondoa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kuhusu parking, nitoe rai kwa Mheshimiwa Mbunge na Halmashauri ya Kondoa kwa kushirikiana na Kamanda wa Zimamoto wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanatenga eneo kwa ajili ya parking ya magari hayo yatakapowasili. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Anatropia Lwehikila Theonest
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka gari la zimamoto Wilaya ya Kondoa ili kukabiliana na majanga ya moto yanayotokea mara kwa mara?
Supplementary Question 2
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Kyerwa ina rekodi ya matukio ya moto ikiwa ni pamoja na shule ya watoto wadogo ambayo imewahi kuungua. Wakati huo huo tunategemea Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kupata gari la zimamoto na ile ni wilaya inayokua kwa kasi. Nataka kujua mkakati wa haraka wa kuhakikisha ile wilaya ina gari la zimamoto.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mji wa Nkwenda, lini itapatiwa gari la zimamoto kwa sababu ni mji unakua, ukiwa na petrol station, kuhakikisha kwamba tunaepusha majanga ambayo yamekuwa yakijitokeza kama siku zilizopita?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu kwenye jibu la msingi, Serikali imeshaagiza magari 150 tayari kwa kusambazwa katika wilaya zote hapa nchini ikiwepo na Wilaya ya Kyerwa. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved