Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ester Alexander Mahawe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTER A. MAHAWE aliuliza:- Wilaya ya Simanjiro haina Hospitali ya Wilaya na hivyo kusababisha mateso kwa wakazi wa maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo hususan wanawake ambao wanakosa huduma za kujifungua lakini pia kutokana na uchache wa vituo vya afya na zahanati. (a) Je, ni lini Serikali itavipa hadhi vituo vya afya vya Mererani na Orkesment ili kupunguza tatizo? (b) Wilaya ya Simanjiro ina gari moja tu la wagonjwa; je, ni lini Serikali itapeleka gari lingine kwenye Kituo cha Afya Mererani ili kuokoa maisha ya akina mama wajawazito?
Supplementary Question 1
MHE. ESTER A. MAHAWE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali langu la kwanza linasema kwamba kuna uhaba mkubwa wa watumishi wa kada ya afya, hasa katika Mkoa wa Manyara kwenye zahanati na vituo vya afya. Je, Serikali ina mkakati gani sasa wa kuhakikisha hilo nalo linatatuliwa?
Mheshimiwa Spika, swali la pili tuna upungufu wa dawa hususan Mkoa wa Manyara kwenye hospitali zake zote Je, Serikali ina mpango gani na hili maana afya za wananchi ziko hatiani? Ahsante sana.
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, katika suala zima la watumishi kama tunavyojua ni kwamba maeneo mbalimbali yanakabiliwa na uhaba wa watumishi, hii tumesema ni commitment ya Serikali. Kama nilivyosema katika jibu wakati namjibu Mbunge wa Handeni kwamba Serikali sasa hivi mchakato wa vibali ukikamilika vizuri katika Ofisi ya Utumishi, basi nadhani tutapeleka watumishi kwa kadri maeneo yote yanayowezekana, especially katika Mkoa wako wa Manyara Mheshimiwa Mbunge.
Mheshimiwa Spika, suala zima la upungufu wa dawa ni kweli na naomba kila Mbunge hapa a-pay attention ya kutosha. Nimepita katika Halmashauri mbalimbali Serikali tumeamua kutoa fedha za basket fund awamu mbili zimekamilika, hivi sasa tumeshapeleka fedha za basket fund katika awamu ya tatu, lakini kwa bahati mbaya sana miaka yote uki-track record fedha za basket fund ambayo inakuonesha one third lazima itumike katika kununua madawa na vifaa tiba katika Halmashauri zetu fedha hizo hazitumiki sawasawa.
Mheshimiwa Spika, maeneo mengine utakuta fedha tumezipeleka lakini wakati natembelea juzi, fedha za awamu ya kwanza na fedha za awamu ya pili utafika katika Halmashauri bado fedha za basket fund kwa ajili ya ununuzi wa madawa na vifaa tiba hazijanunuliwa. Ndiyo maana tumetoa maelekezo kwa DMO wote wahakikishe kwamba fedha zilizopelekwa katika maeneo yao zinaenda kutatua matatizo ya wananchi kama tulivyoelekeza.
Mheshimiwa Spika, hili nimhakikishie Mheshimiwa Ester, juzi nilikuwa naongea na Mkurugenzi wako kule wa eneo lile na kumwelekeza kwamba zile fedha aweze kununua na ameniambia ameshanunua dawa nyingine, lakini kuna dawa zingine bado anaziomba kutoka MSD, kuna dawa zingine ameambiwa hazipatikani na nimewaelekeza kwamba, wafanye utaratibu kuzipata dawa hizo lengo kubwa ni wananchi wa maeneo hayo waweze kupata huduma. Kwa hiyo, ni commitment ya Serikali na tunajitahidi kufanya kila liwezekanalo ili kuondoa hili tatizo la dawa nchini kote.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved