Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rwegasira Mukasa Oscar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Primary Question

MHE. OSCAR R. MUKASA aliuliza:- Mgodi wa Stamigold, Biharamulo uko kijijini Mavota katika Wilaya ya Biharamulo na wananchi wa Kijiji cha Mavota kwa sasa hawana fursa hata kidogo ya kufanya uchimbaji mdogo mdogo licha ya kwamba mgodi huo upo kijijini kwao, hali ambayo imekuwa chanzo kikubwa cha migogoro inayosababisha uvunjifu wa amani:- (a) Je, Serikali iko tayari kuwa na mazungumzo ya kimkakati na wananchi wa Kijiji cha Mavota kupitia Mbuge wao kwa manufaa ya uwekezaji na wanakijiji wa Mavota? (b) Kama Serikali haiko tayari kufanya mazungumzo hayo, je, ni kwa sababu zipi?

Supplementary Question 1

MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri yenye kuakisi nia ya Wizara na Serikali kushirikiana nasi, nina swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye swali la msingi, imeelezwa vizuri kabisa kwamba uvunjifu wa amani ni moja ya matokeo hasi ya kukosekana kwa fursa hizi za wananchi wa Mavota kushiriki kwenye uchumi uliowazunguka. Kwa sababu suala la uvunjifu wa amani si suala la kusuburi, ni la haraka, je, Serikali na Wizara iko tayari kutoa kauli inayothibitisha uharaka wao katika kuja kuzungumza na wananchi wa Mavota?

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba hatua ambazo Serikali imechukua kupitia Wizara yetu ni pamoja na kuhakikisha kwamba uchimbaji salama na makini unafanyika kwenye eneo hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuzingatia umuhimu huo, ofisi yetu iko tayari kwenda kuzumgumza na wananchi kuwahakikishia amani zaidi kwenye shughuli za uchimbaji eneo la Mavota.