Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Lucy Simon Magereli

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. LUCY S. MAGERELI aliluliza:- Katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Tano kumekuwa na mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa shughuli za Bunge kwa kupunguza muda. Bunge sasa hukaa kwa siku 10 hadi 12 tu jambo ambalo linasababisha muda wa kuchangia na Mawaziri kujibu hoja kuendelea kupunguzwa hadi kufika dakika tano tu kitu ambacho kimepunguza kabisa ufanisi wa chombo hiki muhimu chenye majukumu muhimu. Je, Serikali ina mpango gani wa kuliwezesha Bunge kufanya shughuli zake kwa ufanisi kwa kuliongezea bajeti?

Supplementary Question 1

MHE. LUCY S. MAGERELI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Hata hivyo, nieleze masikitiko yangu tu kwamba eti unapata majibu ya Serikali, yanakwambia Mpango wa Serikali kuliwezesha Bunge kufanya shughuli zake kwa ufanisi ni kutoa
fedha toka Mfuko Mkuu wa Serikali kupeleka kwenye Mfuko Mkuu wa Bunge, Fungu 42 eti huo ndiyo mpango.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli sijaridhika na
majibu ya Mheshimiwa Waziri kwa sababu najua sisi wote hapa katika Bunge hili ni mashahidi, majukumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni muhimu na nyeti sana kuliko hiki ambacho Serikali inataka kutuambia kwamba
mpango wake ni kutoa fedha Mfuko Mkuu wa Serikali na kupeleka Mfuko wa Bunge. Ninyi wote ni mashahidi kwamba kwa mujibu wa kanuni, muda wa Kamati za kuelekea bajeti ni wiki tatu lakini this time wiki moja imeondoshwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwenye swali langu la msingi nilichouliza ni kwamba, muda wa uendeshaji wa shughuli za Bunge umepunguzwa mno kiasi cha kufikia siku 10 hadi 12, lakini hata muda wanaopewa Mawaziri kujibu hoja za Wabunge na wananchi wa Tanzania nao
umepunguzwa kufikia kiasi cha dakika tano. Kwa hiyo, hatutekelezi wajibu wetu kama Bunge kwa sababu tunakimbizana na muda ingawa hili la muda naona halikuzingatiwa, lakini bado hoja ya bajeti mpaka mweziwa Pili mmetupa asilimia 68, tu kwa hiyo bado hata hilo ambalo mlifikiri ni kazi rahisi tu kutoa Mfuko wa Serikali kuweka
Mfuko wa Bunge bado hamjatoa kiasi kinachokidhi, bado mnatusafirisha kwenye Hiace, bado…
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa binafsi yangu, naomba nielezwe kabisa straight forward kama hili ndiyo jibu la Serikali basi swali hili halijajibiwa
naomba lijibiwe.

Name

Dr. Philip Isdor Mpango

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

..