Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Deogratias Francis Ngalawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ludewa

Primary Question

MHE. DEO F. NGALAWA Aliuliza:- Shirika la Posta Tanzania lilitumia fedha zake kuwalipa Wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki:- Je, Serikali ina mpango gani wa kulirejeshea Shirika hilo fedha hizo ili kulinusuru?

Supplementary Question 1

MHE. DEO F. NGALAWA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika mwaka 1977, mpaka
leo hii ni miaka 40. Shirika hili limekuwa likisuasua sana lakini moja kati ya vigezo inavyolifanya lisuesue ni kwamba hela yake ambayo ilitakiwa iingie kwenye operesheni ndiyo hiyo ambayo inatumika kuwalipa wale wastaafu wa Afrika Mashariki. Je, Serikali ina mpango gani sasa hivi kuanza kuwalipa wale wastaafu yenyewe moja kwa moja bila kutumia fedha za shirika? Pili, fedha hizi ambazo tayari Shirika la Posta linaidai Serikali ni lini zitakamilishwa kulipwa kwa sababu imefikia kipindi Shirika linasuasua, ikafikia kipindi hata ule mwaka 2016 Shirika hili lilifungiwa akaunti zake kwa sababu TRA ilikuwa inalidai sh. 600,000,000. Je, kulikuwa na fairness gani ya kufungia zile hela wakati shirika hilo linaidai Serikali shilingi bilioni tano?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza Serikali ina mpango gani wa
kulipa yenyewe, naomba kulijulisha Bunge lako Tukufu kwamba Serikali sasa hivi iko kwenye jitihada za kuhakikisha kuwa malipo haya yanalipwa na Serikali yenyewe na kwa kuwa tayari watumishi wote wa Shirika la Posta wanaendelea kuchangia kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, wastaafu hawa wataendelea kulipwa na Mifuko hii badala ya kulipwa tena na Shirika la Posta.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ni lini fedha hizi zitalipwa. Kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi kwamba, tutaendelea kulipa kwa kadri fedha zinapopatikana na ni jukumu la Serikali kulipa fedha hizi tunafahamu, tumejipangia mpango itakapofika Juni 30, shilingi bilioni 3.2 zote zitakuwa zimeshalipwa.