Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Zuberi Mohamedi Kuchauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:- Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC) lililokuwa na matawi karibu nchi nzima na assets mbalimbali lilibinafsishwa kutokana na sera ya ubinasfishaji. (a) Je, ni matawi mangapi yamebinafsishwa na mangapi yamebaki mikononi mwa Serikali? (b) Je, Serikali imepata fedha kiasi gani kutokana na ubinafsishaji huo? (c) Kati ya matawi yaliyobinafsishwa ni mangapi yanaendeshwa kwa ubia wa Serikali?

Supplementary Question 1

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Niseme tu nasikitika kwa majibu ambayo ni rahisi, majibu mafupi, majibu ambayo hayaoneshi matumaini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo Mheshimiwa Naibu Waziri...
...anasema ubinafsishaji wa matawi 22 yaliyokuwa National Milling tumepata shilingi bilioni 7.4, ni masikitiko makubwa sana; na hii inaonyesha moja kwa moja kwamba sisi huu umasikini umetuandama. kwa sababu kama tunaweza tukatupa…
..ni masikitiko makubwa sana. Msheshimiwa Mwenyekiti, najenga hoja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna matawi kama Plot 33, Plot 5, Tangold yale matawi sasa hivi yote ni ma-godawn. Watu walionunua matawi ya National Milling ambayo yanafanya kazi ni Bakheresa na Mohamed Enterprises peke yake, lakini matawi mengine yote yaliyobaki yamekuwa ma-godawn na ninyi mnasema mnaenda kwenye viwanda, mimi hapa sijapata kuelewa. Nini hatima ya hayo mashirika ambayo sasa hivi ni ma- godawn badala ya kuwa viwanda? (Makofi)
(b) Kwanza niseme wazi kwamba na mimi ni mmoja kwenye taaluma hii ya usindikaji wa nafaka. Nimefanya kazi National Milling si chini ya miaka 10. Kwa upande wa Kurasini mnamo tarehe 31 Aprili, 2005 waliletewa barua aliyekuwa Meneja pale kwamba kiwanda hicho akabidhiwe Mohamed Enterprises anayekaribia kununua, alikabidhiwa tu kwa sababu anakaribia kununua. Si hivyo tu, wafanyakazi waliokuwepo pale mpaka leo hii wanaidai Serikali hii zaidi ya shilingi milioni 234.3, bado hatima yao haieleweki na kesi imekwisha. Vilevile si hivyo tu, tarehe 20…Hazina wameitwa mahakamani hawataki kwenda, nini hatima ya wafanyakazi wale?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza nini hatima ya hayo Mashirika ambayo yalikodishiwa na sasa sio viwanda ni ma- godown. Naomba kumkumbusha Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ilishaanza mchakato wa kufanya tathimini ya viwanda vyote vilivyouzwa na ambavyo vimegeuzwa matumizi.
Mheshimiwa Waziri wa Viwanda alishasimama hapa na kusema na ndiyo kauli ya Serikali, kwamba vyote hivyo vitarejeshwa Serikalini na vitaendelea kufanya kazi, na vitatafutiwa wawekezaji na wataendelea kuviendesha viwanda hivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili linalohusu hatima ya wafanyakazi, ameshasema kesi iko mahakamani, ikishakuwa mahakamani naomba nisiliongelee hapa na ni imani yangu kwamba kesi hiyo itaendeshwa na itafika mwisho mzuri.