Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Daimu Iddi Mpakate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kusini

Primary Question

MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza:- Katika upande wa kusini mwa Jimbo la Tunduru Kusini wananchi takribani 200 wa Tanzania na Msumbiji huvuka Mto Ruvuma kila siku kutafuta mahitaji yao ya kila siku, upande wa Msumbiji wameweka Askari wa Uhamiaji ambao huwanyanyasa sana Watanzania kwa kuwapiga na kuwanyang’anya mali zao kwa kukosa hati ya kusafiria. Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka Kituo cha Uhamiaji katika kijiji cha Makande Kazamoyo na Wenje ili kuwapatia Watanzania huduma ya uhamiaji?

Supplementary Question 1

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu mazuri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-
Kwa kuwa Serikali imetambua urefu mkubwa uliopo kutoka Ofisi ya Uhamiaji ilipo mpaka Wenje, Makande na Kazamoyo; na kwa kuwa wananchi hawa wa maeneo haya hawana uwezo mkubwa wa kuweza kufuata huduma hii ya uhamiaji zaidi ya kilometa 90 ziliko ofisi; na kwa kuwa Serikali inakosa mapato kutokana na tozo zinazotolewa kwenye hati hizi ya kusafiria; je, kwa nini Serikali haioni umuhimu kwa sasa wa kuweza kutoa huduma hii kwa njia ya mobile ili wananchi hawa waweze kupata huduma hii kwa haraka?
Swali la pili, katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
Ofisi ya Uhamiaji ina gari ambalo kwa muda mrefu ni bovu halina huduma yoyote katika maeno yote yaliyopo. Je, Serikali ni lini itatoa gari kwa ajili ya kurahisisha huduma hii ili wananchi wale wahudumiwe kwa urahisi zaidi?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kukosa mapato Serikali si hoja ya kukosekana kituo karibu na mpaka. Kwa sababu kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiji namba 54 pamoja na Kanuni zake mwaka 2015, inaeleza kabisa kwamba ili mtu aweze kuvuka kutoka nchi yetu na kwenda nchi nyingine anahitaji kuwa na nyaraka za aina tatu.
Nyaraka hizo aidha ni passport ama hati ya dharula ya kusafiria ama kibali maalum. Kwa hiyo, kwa mwananchi yoyote anahitaji kuvuka lazima apitie katika njia hizo whether ofisi ipo katika mpaka, ofisi ipo katika Wilaya ama ofisi iko katika Mkoa, kwa hiyo hiyo naona ni hoja ambayo siyo sahihi, ninaomba Mheshimiwa Mbunge aendelee kuwasisitiza wananchi wake juu ya umuhimu wa kuweza kutii sheria za nchi yetu ili kuepusha uvukaji wa mipaka kiholela na kuikosesha Serikali mapato.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kuhusiana na gari, hili naomba Mheshimiwa Mbunge atuachie tulichukue, kwa sasa hivi hatuna gari za kutosha kwa Uhamiaji, pale ambapo gari zitapatikana tutaangalia na changamoto zingine za maeneo mengine na vipaumbele vilivyopo ili tuzingatie na kuchukua hatua stahiki.