Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Oran Manase Njeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbeya Vijijini

Primary Question

MHE. ORAN M. NJEZA (K.n.y. MHE. RIDHIWANI J. KIKWETE) aliuliza:- Hivi karibuni kumetokea mapigano baina ya wakulima na wafugaji ambayo yamesababisha baadhi ya Watanzania kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa maisha:- Je, Serikali imejipangaje kupambana na janga hilo?

Supplementary Question 1

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Kwa ajili ya matatizo ya migogoro ya wafugaji na wakulima, maeneo mengi yanahitaji sasa hivi kuwe na vituo vidogo vya Polisi. Je, Serikali au Wizara inatupa commitment gani kuwa kutakuwa na vituo vya Polisi katika maeneo hayo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa wananchi wamekuwa wakijitolea kujenga vituo vya Polisi kama ilivyokuwa kwa kituo cha Polisi cha Wilaya ya Mbeya ambao wamejenga kwa asilimia karibu zaidi ya 50. Je, Serikali inawaahidi nini wale wananchi wa Mbalizi kuwaunga mkono kuwamalizia kile kituo chao cha Polisi? Ahsante.

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpe pole Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete kwa kupatwa na msiba na ndiyo maana hajaweza kuwepo kuuliza swali. Mungu ampe moyo wa ustahimilivu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la nyongeza alilouliza Mheshimiwa Oran; moja kituo cha Mbeya ambacho wameshafanya kazi kubwa sana nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa sababu amefanya hamasa kubwa sana na najivunia kwamba nilikwenda kumuunga mkono wakati wa kampeni. Kwa kuwa amefanya kazi kubwa sana na sisi kama Wizara tuna bajeti ambayo tumetenga kwa ajili ya umaliziaji wa majengo ambayo yameshafikia hatua kubwa. Hivyo, tutafanya ziara, tutajionea na tutaweka wataalam ili waweze kukadiria na kwenda kwenye utekelezaji wa umaliziaji ili nguvu ya wananchi isiweze kupotea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ujenzi wa vituo karibu na maeneo ambayo yanakuwa na migogoro ya mara kwa mara, Serikali inaendelea kufanya utaratibu wa kuweza kuwepo vituo hivyo lakini pale ambapo vituo hivyo havipo tutaendelea kufanya doria ili kuweza kuhakikisha kwamba tunawahakikishia wananchi usalama wao punde panapokuwepo na migongano ya aina hiyo hata kama bado hatujaweka vituo vya Polisi.