Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Juma Othman Hija
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tumbatu
Primary Question
MHE. JUMA OTHMANI HIJA aliuliza:- Kumekuwa na matukio yasiyo ya kawaida na kukaribia kuhatarisha amani katika Kisiwa cha Tumbatu:- Je, Serikali haioni ipo haja ya kujenga Kituo cha Polisi katika Kisiwa hicho ili kukabiliana na matukio ya kiuhalifu?
Supplementary Question 1
MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina swali moja la nyongeza.
Katika majibu yake ya msingi anasema kwamba Serikali inakamilisha mipango ya kupata fedha ya kujenga kituo hiki. Je, anaweza kutuambia kwa kiasi gani mipango hii imefikia? Under what percentage imefikia? Ahsante.
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO NA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nimejibu katika swali langu la msingi ni kwamba wakati Serikali inajipanga kuweza kuanza mchakato wa ujenzi wa Kituo cha Polisi Tumbatu, tayari kuna jitihada mbalimbali ambazo zimeshachukuliwa kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yale. Ukiachia mbali jitihada ambazo nimezijibu katika swali la msingi za kuhakikisha kwamba tunaendeleza kupeleka askari wa doria mara kwa mara, lakini pia sasa hivi karibu na eneo la Tumbatu kwenye eneo la Mkokotoni kuna ujenzi wa Kituo cha Polisi Mkokotoni ambapo kiko katika hatua za mwisho kukamilika.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika bajeti ya mwaka huu tumetenga fedha takribani shilingi milioni 200 kwa ajili ya kulimpa mkandarasi ili aweze kuendelea na kukamilisha kituo hicho ambacho kipo katika hatua ya mwisho. Tunaamini kabisa kwamba Kituo cha Mkokotoni kikimalizika, kitasaidia sana kuweza kusogeza karibu na Tumbatu huduma za polisi wakati ambapo jitiahada za ujenzi wa Kituo cha Tumbatu zikiwa zinaendelea.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved