Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Prof. Norman Adamson Sigalla King
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING aliuliza:- Utafiti uliofanywa na Serikali unaonesha kuwa Mto Lumakali unaozalisha maji katika Wilaya ya Makete unaweza kuzalisha megawatts 640 za umeme na hasa ikizingatiwa kuwa Wilaya ya Makete inapata mvua kwa miezi nane (8) kwa mwaka:- Je, ni lini ujenzi wa bwawa ambao ni mpango wa Serikali wa tangu mwaka 2005 utaanza ili kusaidia kujenga uchumi wa kudumu huko Makete, Mkoa wa Njombe na Mbeya kwa ujumla?
Supplementary Question 1
MHE. PROF. NORMAN A. S. KING: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu ya Naibu Waziri yanayoleta matumaini. Hata hivyo, nina maswali madogo ya nyongeza. Kwa kuwa mradi huu ulitegemewa kuzalisha umeme na wananchi wote wa Tanzania kunufaika, ni lini sasa Serikali itapeleka umeme kwenye vijiji 76 ambavyo havina umeme Wilaya ya Makete? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ni lini Serikali itakamilisha upelekaji wa umeme kwenye vitongoji ambavyo havikupata umeme Awamu ya Kwanza ya REA? (Makofi)
Name
Dr. Medard Matogolo Kalemani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chato
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Profesa anavyotupa ushirikiano katika jimbo lake na awali ya yote nimhakikishie vijiji vyake 76 vitapata umeme kwenye Awamu ya Tatu ya REA inayoanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini sasa vijiji vilivyobaki vitapelekewa umeme, katika majibu yetu ya kila siku tumekuwa tukisema Mradi wa REA Awamu ya Tatu umeanza tangu mwezi Machi, 2017 na vijiji vyote vilivyosalia pamoja na vya Mheshimiwa Profesa King vya Makete pamoja na maeneo mengine vitapelekewa umeme kati ya mwaka huu wa 2017 hadi 2020. Kwa hiyo, Mheshimiwa Profesa, vijiji vyake vyote vitapata umeme.
Mheshimiwa Mwenyekiti, natambua sana Kata za Mang’oto, Lupende, Kambata na Mabacha pamoja na maeneo mengine ambayo anayataja yatapatiwa umeme katika awamu hii. Vilevile vitongoji na taasisi zake za umma vitapatiwa umeme na mradi huo ni mmoja umeshaanza, tumezindua kwa Mkoa wa Iringa na Njombe kwa Mheshimiwa Mbunge wa Kilolo na kwake wameshaanza, naambiwa wiki ijayo watafika kwa Mheshimiwa Profesa.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved