Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Elibariki Emmanuel Kingu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Magharibi

Primary Question

MHE. ELIBARIKI E. KINGU aliluliza:- Wilaya ya Ikungi hasa Jimbo la Singida Magharibi inakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa vituo vya afya na zahanati. Aidha, umbali mrefu wa kutafuta matibabu umekuwa ukisababisha adha na taabu kwa wananchi wa kata za Lyandu, Igelansomi na vijiji vya Mduguya, Kaangeni, Chengu na Mayahu. Je, Serikali ipo tayari kushirikiana na wananchi katika kukamilisha ujenzi wa zahanati mpya na vituo vya afya vilivyoanzishwa kwa ushirikiano wa wananchi na Mbunge?

Supplementary Question 1

MHE. ELIBARIKI E. KINGU: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya kaka yangu Mheshimiwa Jafo, nilikuwa nataka nipate hakikisho kwa sababu hivi tunavyozungumza mimi na wananchi tumeanzisha ujenzi wa zahanati katika vijiji 19 kwa nguvu zetu.
Mheshimiwa Spika, sasa Mheshimiwa Naibu Waziri atanihakikishia kwamba zahanati hizi za Nkunikana, Puma, Msambu, Unyangwe, Chungu, Kinyampembee, Mpetu, Mayaha, Misake, Maswea, Nsogandogo, Kipunda, German, Mahonda, Iyumbu, Mlandala, Kaugeri, Mduguyu, Mpugizi na Namnang’ana ambazo tumezianzisha kuzijenga ndani ya kipindi cha miaka miwili katika huu mgao, Mheshimiwa Naibu Waziri ananihakikishia kwamba na zenyewe zinakwenda kukamilishwa? Hizi ambazo tumezianzisha sisi.

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwanza kama nilivyosema pale awali, napenda kumpongeza sana Mheshimiwa Kingu kwa kazi kubwa anayofanya katika ile Wilaya yote ya Ikungi kwa ujumla wake.
Mheshimiwa Spika, katika mpango wa bajeti wa mwaka huu tumetenga karibuni shilingi bilioni 251 katika Local Government Development Grants, lakini katika hizo karibu shilingi bilioni 68 kwa ajili ya kuboresha vituo vya afya na zahanati, yaani yale maboma yaliyojengwa. Katika hizo nilisema pale awali 1.4 billion ni kwa ajili ya Halmashauri ya Ikungi.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba tu Kamati ya Fedha itakapokaa pale, katika vipaumbele vya umaliziaji wa maboma, haya maeneo ambayo tumesema tutawaletea fedha, basi ni vyema katika ule mpango ni lazima tuhakikishe maboma haya yamekamilika kwa sababu Serikali ndiyo imeshafanya jambo lake hilo.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, Mheshimiwa Kingu alileta concern kubwa ya Halmashauri yake kuhusu changamoto ya afya. Ndiyo maana kama Serikali kwa ujumla, hivi sasa tunawapelekea fedha za kwanza, karibu shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya pale Ihanja ambapo tunajua pale kutakuwa na theater kubwa na maabara. Kwa hiyo, eneo lile litabadilika.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kutakuwa na fedha nyingine kwa ajili ya ununuzi wa vifaa. Kwa hiyo, Serikali iko tayari kuhakikisha kwamba wananchi wa Halmashauri yote ya Ikungi inapata huduma nzuri kama tunavyotarajia.

Name

Yahaya Omary Massare

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Magharibi

Primary Question

MHE. ELIBARIKI E. KINGU aliluliza:- Wilaya ya Ikungi hasa Jimbo la Singida Magharibi inakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa vituo vya afya na zahanati. Aidha, umbali mrefu wa kutafuta matibabu umekuwa ukisababisha adha na taabu kwa wananchi wa kata za Lyandu, Igelansomi na vijiji vya Mduguya, Kaangeni, Chengu na Mayahu. Je, Serikali ipo tayari kushirikiana na wananchi katika kukamilisha ujenzi wa zahanati mpya na vituo vya afya vilivyoanzishwa kwa ushirikiano wa wananchi na Mbunge?

Supplementary Question 2

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona. Matatizo yaliyoko huko Singida Magharibi yanafanana kabisa na yaliyoko katika Jimbo la Manyoni Magharibi, na sisi tumeanza kujenga zahanati nyingi.
Je, Serikali iko tayari sasa kuiongezea mgao Halmashauri ya Itigi ili iweze kufunika maboma ambayo tayari tumeshayaanza katika vijiji vya Mbugani, Mnazi Mmoja, Tulieni na vijiji vingine vingi?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, ni kweli anachoshuhudia Mheshimiwa Mbunge kwamba tulipofika pale Itigi katika Halmashauri ya Itigi, lakini bahati mbaya wao hawana Hospitali ya Wilaya. Ndiyo maana mpango wa Serikali ni kuhakikisha kwamba Halmashauri ile ambayo kwa jiografia yake mara nyingi wanatumia kile Kituo cha Kanisa kama ndiyo sehemu kubwa ya utoaji huduma ya afya, Serikali hatutasita kutoa ushirikiano.
Mheshimiwa Spika, katika ule mpango ambao fedha ambazo tumetenga; na Halmashauri hiii tutaipa kipaumbele. Kwa hiyo, Mkurugenzi ahakikishe yale maboma yaliyoanzwa kujengwa, yamemilika. Hata hivyo, kuna mpango kwamba, tutaisaidia Itigi as a special case kuona ni jinsi gani wananchi wa Manyoni Magharibi wataweza kupata huduma nzuri.