Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Rashid Abdallah Shangazi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mlalo
Primary Question
MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaharakisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Kata za Manolo, Shume, Sunga na Mbaru ili kuwaondolea usumbufu Wananchi wa maeneo hayo ikiwemo ushiriki hafifu kwenye shughuli za kiuchumi?
Supplementary Question 1
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kuniona. Pamoja na majibu mazuri yenye kutia matumaini ya Naibu Waziri, naomba niulize swali la nyongeza kama ifuatavyo:-
Je, ni lini Serikali itakuja na mpango wa muda mfupi wa kuwapatia japo huduma ya visima virefu wakazi wa vijiji vya Maseleka, Madala na Tema wakati wanasubiri utekelezaji wa mradi huu mkubwa? Ahsante.
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, kwanza Mheshimiwa Shangazi nadhani ni Mbunge kijana na ni mara yake ya kwanza ameingia Bungeni lakini ameonesha ni wazi kwamba kuingia kwake moja kwa moja ameenda katika ajenda kubwa ya suala zima la matatizo ya wananchi kuhusu suala la maji.
Mheshimiwa Spika, kutokana na ajenda hiyo naomba Serikali ichukue wazo hili, naomba tuangalie kwamba ni jinsi gani tutafanyakazi kwa pamoja ili wananchi wa Mlalo waweze kupata huduma hii ya maji. Naomba nichukue jambo hilo na naomba nimuahidi kwamba Ofisi yetu, Mheshimiwa Waziri wangu nadhani ataniruhusu nitafika kule Mlalo, licha ya ajenda ya maji nadhani ana changamoto nyingi kama Mbunge kijana lazima tumsaidie ili Jimbo lake liende vizuri.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved