Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Silvestry Fransis Koka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibaha Mjini

Primary Question

MHE. SILVESTRY F. KOKA aliuliza:- Mradi wa umeme wa 400KV wa kutoka Kinyerezi hadi Arusha ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi na Taifa letu; kuanzia mwaka 2015 wananchi wa maeneo ya Kibaha Mjini ambako mradi huu unapita wamechukuliwa maeneo yao na yalifanyiwa uthamini kwa ajili ya wananchi kulipwa fidia:- Je, ni lini fidia hii italipwa kwa wananchi walioathirika na mradi huu?

Supplementary Question 1

MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Nabu Spika, nakushukuru na namshukuru Mheshimiwa Waziri na Serikali kwa jitihada kubwa ya kusambaza umeme. Pamoja na hayo nina maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, toka mradi huu ulipoanza na wananchi kufanyiwa tathmini ni takribani miaka mitatu na wananchi hawa wameacha shughuli zao za maendeleo na hawana fedha kwa ajili ya kuanzisha shughuli nyingine ya maendeleo. Ni lini sasa Serikali itaanza kulipa fidia hii ili wananchi wajiandae kwa ajili ya kuwa na shughuli za maendeleo mbadala katika maeneo mengine?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; katika mradi wa umeme REA III, Vijiji vya Jimbo la Kibaha Mjini ikiwa ni pamoja na Mkombozi, Lumumba, Kalabaka, Saeni, Jonuga, Mbwawa, Miomboni, Madina, Mbwate, Visiga, Viziwaziwa, Mtakuja, Maili 35 na Kumba vimeondolewa katika utaratibu mzima wa REA III na katika kufuatilia kwangu hatujapata majibu ni utaratibu gani utatumika kuipatia Mitaa hii umeme kama ilivyokuwa imepangwa na wananchi wana mtafaruku mkubwa. Je, Serikali sasa ina mpango gani mbadala kuhakikisha mitaa hii yote inaendelea kupata umeme kama tunavyojua umeme ni uchumi na maendeleo?

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa Mheshimiwa Koka hongera sana katika kufuatilia masuala ya fidia. Mmefika hatua nzuri kwa sababu ya jitihada zako.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa kwamba katika maeneo yaliyofanyiwa tathmini kama nilivyoeleza kwenye swali langu na jibu langu la msingi kwamba taratibu zimeshakamilika na ni matarajio yetu mwisho wa Desemba na mwanzo wa Januari mwakani, malipo yatakuwa yameshaanza kutoka. Kwa hiyo, wananchi wa maeneo yale wategemee fidia katika kipindi hicho, lakini kama nilivyosema, taratibu za uhakiki zimeshakamilika.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili; nitumie nafasi hii kusema kwamba yako maeneo ambayo kwa kweli ni mitaa ingawa katika hali ya kawaida inaonekana kama vijiji. Maeneo haya ambayo yako mjini kwa sababu miradi ya REA inakwenda vijijini, uko mradi unaoitwa urban ratification ambao katika Wilaya ya Kibaha hasa Mjini na maeneo ya jirani yatapelekewa umeme kupitia mradi huu. Mheshimiwa Koka kwa bahati nzuri sana, katika maeneo ya Lumumba, Mtakuja na Viziwaziwa ziko transformer 11 zimetengwa kwa ajili yakupelekewa umeme katika maeneo hayo.