Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Joseph Kizito Mhagama
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Madaba
Primary Question
MHE. JOSEPH K. MHAGAMA aliuliza:- Zaidi ya wananchi 181 wa kijiji cha Ngadinda Halmashauri ya Madaba wanalima ndani ya Wilaya ya Namtumbo kwa sababu ya kukosa eneo katika kijiji chao. Baraza la Madiwani lilishauri sehemu ya shamba la hekta 6,000 la Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi lililopo ndani ya kijiji hicho ambalo lilikabidhiwa kwa Halmashauri ya Wilaya ili litumike kwa shughuli za kilimo na sehemu ibaki kwa ajili ya mifugo. Hivi sasa wafugaji toka maeneo mbalimbali nchini wapo katika shamba hilo lakini wakulima hawajatengewa eneo. (a) Je, Serikali haioni kwamba kitendo hicho ni ubaguzi na kinaweza kuchochea migogoro kati ya wafugaji na wakulima? (b) Je, ni lini Serikali itasikiliza kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Ngadinda cha kutengewa eneo la kilimo?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPH K. MHAGAMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafsi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa vile vikao halali vya Halmashauri ya Wilaya ya Songea vilishamaliza jukumu la kihalmashauri kuhusu matumizi ya eneo hili la ardhi; na kwa vile katika mazungumzo na ufuatiliaji Wizara ya Kilimo walishaelekeza kwamba sasa Mkoa ukabidhi sehemu ya eneo la shamba hilo kwa wananchi ili waweze kuendelea na shughuli za kilimo; na kwa vile msimu wa kilimo umekaribia sana na wananchi hawana sehemu ya kulima mazao ya chakula, na kwa vile wafugaji tayari wameanza kufuga katika eneo hilo.
Je, Serikali ipo tayari sasa kutoa maelekezo kwa Serikali ya Mkoa kuhusu kutekeleza jukumu hili haraka iwezekanavyo?
Pili, iwapo zoezi hili litaendelea kuchelewa kutekelezwa, je, Serikali ipo radhi sasa kuruhusu wananchi wa Ngadinda na kwa vile mipaka inafahamika, kuiagiza Serikali ya kijiji iweze kuanza kushirikiana na wananchi kuwatengea maeneo hayo waweze kuanza kuzalisha?
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa hizo initiative zote walizozifanya mpaka wamefikia hapo. Mimi nafahamu kwamba kama hatua nyingi za msingi zimeshafanyika kikubwa zaidi ni sehemu yetu ya Mkoa. Nichukue fursa hii kuiagiza Ofisi ya Mkoa wa Ruvuma iangalie jinsi gani ya kufanya kama mijadala yote imeshakamilika iende haraka kurekebisha jambo hili ili wakulima na wafugaji tusiwe na mgogoro tena katika eneo hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunajua wazi kwamba jambo hili likiwa na ukakasi wake mwisho wa siku tunakuja kuzalisha matatizo makubwa sana ya uvunjivu wa amani. Kwa hiyo, nitumie fursa hii kuiagiza timu ya Mkoa wetu wa Ruvuma iende ikalifanyie kazi jambo hilo haraka iwezekanavyo na ikiwezekana mpaka mwezi wa Kumi jambo hilo liwe limekamilika na ofisi yetu ya TAMISEMI tupate taarifa ya jinsi gani jambo hilo limekamilishwa kwa sababu vikao vyote halali kwa taarifa niliyoipata kutoka kwa Mbunge zimeshakamilika.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika eneo la pili kwamba kukiruhusu kijiji kwenda kuhakikisha kwamba wanaenda kugawa hilo eneo, naomba tuvute subira kwanza, timu ya Mkoa ifanye kazi yake vizuri baadaye tukishapata taarifa tutajua nini kifanyike. Lengo kubwa kama unavyowapigania wananchi wako Serikali itaingilia kati kwa nguvu zote sisi tukishirikiana na Wizara ya Kilimo tutafanya kila liwezekanalo eneo lile liwe katika utaratibu mzuri, wananchi wa eneo lile waweze kupata ardhi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ondoa hofu Mheshimiwa Mbunge tunalifanyia kazi jambo hili.(Makofi)
Name
Anne Kilango Malecela
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Same Mashariki
Primary Question
MHE. JOSEPH K. MHAGAMA aliuliza:- Zaidi ya wananchi 181 wa kijiji cha Ngadinda Halmashauri ya Madaba wanalima ndani ya Wilaya ya Namtumbo kwa sababu ya kukosa eneo katika kijiji chao. Baraza la Madiwani lilishauri sehemu ya shamba la hekta 6,000 la Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi lililopo ndani ya kijiji hicho ambalo lilikabidhiwa kwa Halmashauri ya Wilaya ili litumike kwa shughuli za kilimo na sehemu ibaki kwa ajili ya mifugo. Hivi sasa wafugaji toka maeneo mbalimbali nchini wapo katika shamba hilo lakini wakulima hawajatengewa eneo. (a) Je, Serikali haioni kwamba kitendo hicho ni ubaguzi na kinaweza kuchochea migogoro kati ya wafugaji na wakulima? (b) Je, ni lini Serikali itasikiliza kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Ngadinda cha kutengewa eneo la kilimo?
Supplementary Question 2
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu wananchi wa Madaba wameonesha kuhamasika sana kulima tangawizi, hata mimi ninalima tangawizi Madaba. Je, Serikali haioni kwamba kiwanda cha Mamba Miamba ambacho kitakuwa tayari by March next year, kitahitaji tangawizi nyingi sana siyo kutoka Same tu pamoja na Madaba.
Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwapatia wananchi wa Madaba ardhi ya uhakika ili walime tangawizi kwa wingi? (Makofi)
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tuchukue kilio cha mama vilevile kama kilio cha Mheshimiwa Joseph Mhagama. Serikali inaona umuhimu huo na tutafanya kila liwezekanalo kuhakikisha mambo pale yanakaa sawasawa wananchi walime tangawizi waje, kulisha katika kiwanda cha Mama Anne Kilango Malecela. (Makofi
Name
Mbaraka Kitwana Dau
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Primary Question
MHE. JOSEPH K. MHAGAMA aliuliza:- Zaidi ya wananchi 181 wa kijiji cha Ngadinda Halmashauri ya Madaba wanalima ndani ya Wilaya ya Namtumbo kwa sababu ya kukosa eneo katika kijiji chao. Baraza la Madiwani lilishauri sehemu ya shamba la hekta 6,000 la Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi lililopo ndani ya kijiji hicho ambalo lilikabidhiwa kwa Halmashauri ya Wilaya ili litumike kwa shughuli za kilimo na sehemu ibaki kwa ajili ya mifugo. Hivi sasa wafugaji toka maeneo mbalimbali nchini wapo katika shamba hilo lakini wakulima hawajatengewa eneo. (a) Je, Serikali haioni kwamba kitendo hicho ni ubaguzi na kinaweza kuchochea migogoro kati ya wafugaji na wakulima? (b) Je, ni lini Serikali itasikiliza kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Ngadinda cha kutengewa eneo la kilimo?
Supplementary Question 3
MHE. MBARAKA K. DAU: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru kwa fursa hii.
Tatizo la mgogoro wa shamba la Madaba linafanana sana na tatizo la shamba la Kigomani na Utumaini lililopo Wilayani Mafia.
Je, Mheshimiwa Naibu Waziri atakuwa tayari kuja Mafia kukaa na wadau wa Halmashauri pamoja na Viongozi wengine kutatua tatizo hilo?
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Mbunge na lile deni letu tumeshatoa shilingi milioni 50 tumemaliza kituo cha afya, hongera sana Mheshimiwa Mbunge kwa ujenzi wa theatre. Hata hivyo, katika jambo hili mimi naomba nilichukue, lakini kabla mimi sijaja kule nimuagize Mkuu wa Wilaya ya Mafia kwanza aende akalishughulikie jambo hili na ikiwezekana tupate taarifa amelishughulikia vipi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nitakapopata hiyo taarifa jinsi gani limeshughulikiwa jambo hili na mgogoro huo haukuisha, na mimi nitaona jinsi gani ya kufanya, lakini kwamba nitatumia vyombo vyangu vya chini kule kwanza, Mkuu wa Wilaya ya Mafia aanze kuifanya kazi hiyo harka iwezekanavyo kumaliza hilo tatizo na ofisi yetu ipate taarifa ndani ya mwezi mmoja, jinsi gani mgogoro huo umeshughulikiwa kwa kadiri iwezekanavyo. (Makofi)