Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Maftaha Abdallah Nachuma
Sex
Male
Party
CUF
Constituent
Mtwara Mjini
Primary Question
MHE. MAFTAHA A. NACHUMA aliuliza:- Mafuriko yanayotokea Mtwara Mjini kila mwaka hasa katika Kata ya Shangani, Cuono, Magomeni na Ufukoni yanasababishwa namiundombinu mibovu ambayo imejengwa chini ya kiwango katika maeneo mengi ya Mji wa Mtwara:- (a) Je, Serikali iko tayari sasa kujenga upya mitaro, madaraja pamoja na miundombinu mingine ili maji yaweze kusafiri kuelekea baharini wakati wa masika? (b) Je, ni lini Serikali itaanza kujenga barabara ya Mikindani - Lwelu ufukweni mwa bahari kwa kiwango cha lami ikizingatiwa kuwa barabara hiyo iko ndani ya Manispaa?
Supplementary Question 1
MHE ABDALLAH N. MAFTAHA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.
(a) Kwa kuwa Mtwara Mjini kila kipindi cha masika maji huwa yanajaa na mafuriko yanatokea na Serikali inatoa kilo 16 za unga, je, Serikali iko tayari hivi sasa kusema tarehe ngapi itaanza ujenzi wa miundombinu Mtwara Mjini?
(b) Kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri kadanganywa katika jibu lake nililiouliza kwamba Barabara ya Mikindani- Lwelu itajengwa lini kwa kiwango cha lami, yuko tayari hivi sasa kufuatana na mimi kama Mbunge ili aweze kujionea mwenyewe kwamba kadanganywa? Ahsante
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, suala la lini barabara hii itajengwa nadhani katika jibu langu la msingi nimesema. Katika Mradi ule wa Strategic City ambapo lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba tuna maeneo mbalimbali ya miji ambayo imejengwa miradi hii, hata ukiangalia pale Tanga, ukiangalia Mbeya ukiangalia Arusha, huu ndiyo mpango mkakati, hivi sasa tunakwenda hata katika Jiji la Dar es Salaam. Eneo hili nimesema kwamba mchakato wake sasa uko katika hali ya manunuzi, lengo ni kwamba bajeti hii sasa mchakato utakapokamilika maana yake miundombinu inakwenda kujengwa. Lakini kusema kwamba nimedanganywa au vipi nitafika kule Mtwara, naomba nikwambie Mheshimiwa Mbunge, siyo Mtwara peke yake, nitahakikisha maeneo yote, ikiwemo na Mtwara niende nikakague maeneo ya field, hii ndiyo kazi kubwa tumekuwa tukiifanya.
Mheshimiwa Naibu Spika, lengo letu ni kuweza kufika kila maeneo kubaini changamoto mbalimbali na hasa katika kipindi hiki mvua inanyesha, maeneo mengi sasa hivi yameharibika. Taarifa ya habari pale ukiangalia jana Kyela, ukiangalia Morogoro na maeneo mbalimbali yameharibika. Kwa hiyo, ni jukumu la Ofisi hii, kufika kila mahali kubaini uhalisia wa eneo lile wananchi waweze kupata huduma inayokusudiwa na Serikali yao.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved