Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO (K.n.y. MHE. LUCY S. MAGERELI) aliuliza:- Askari wa JWTZ wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi kwa kutesa raia na saa nyingine Jeshi la Polisi. Matukio haya yamekuwa yakifanyika maeneo ya starehe, kwenye foleni za magari, mitaani na katika magari ya usafiri wa umma. Hivi karibuni Mkoani Tanga, kijana mmoja kondakta wa daladala alimzuia mtoto wa mwanajeshi kupanda daladala yake bila nauli, alikamatwa na kuteswa na wanajeshi ndani ya Kambi, kitu kilichopelekea kifo chake. (a) Je, sheria ipi inawapa wanajeshi haki ya kutesa raia? (b) Je, Serikali inachukua hatua gani kukomesha hali hii?

Supplementary Question 1

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mimi ni Mheshimiwa Paresso, kwa niaba ya Mheshimiwa Magereli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.
Kwa kuwa ni ukweli kwamba hakuna aliye juu ya sheria lakini wakati mwingine wanajeshi wetu baadhi wamekuwa wakijiona kwamba wao ni superior kuliko watu wengine; je, Wizara ina mkakati gani wa kuendelea kutoa elimu ili wanajeshi hao wafuate sheria na kujenga mahusiano mazuri kati ya wananchi na jeshi?
Swali la pili, pia kumekuwa na mahusiano hafifu kati ya jeshi na wananchi hasa katika yale maeneo ambao yana migogoro ya ardhi. Je, Wizara sasa ipo tayari kuhakikisha migogoro hii inaisha kwa wakati ili mahusiano haya yaendelee kuimarika?

Name

Dr. Hussein Ali Mwinyi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwahani

Answer

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati wa kutoa elimu upo. Wanajeshi mara zote wamekuwa wakikumbushwa kuishi vizuri na raia hususan wale wanaowazunguka katika makambi yao. Mara kwa mara zimekuwa zikichukuliwa hatua za kinidhamu ndani ya vikosi vyetu vya jeshi pale wanapokiuka utaratibu huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima tueleze vilevile kwamba sheria za nchi hii zinataka mtu anapohisi amevunjiwa haki yake, basi ana haki ya kwenda kushtaki. Kwa kuwa wanajeshi hawako juu ya sheria, sheria hufuata mkondo wake. Kwa hiyo, hilo lizingatiwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mahusiano hafifu kwenye migogoro ya ardhi, hili napenda niliseme, kama tulivyoeleza wakati tunatoa bajeti yetu hapa, kwamba juhudi zote zinafanyika ili migogoro ya ardhi inayohusisha Kambi za Jeshi iweze kuisha. Yapo maeneo ambayo wananchi wamevamia maeneo ya jeshi, kwa hiyo, ni vizuri wananchi nao wakapewa elimu hiyo hiyo ili wasiweze kuvamia maeneo ya jeshi. Kwa yale maeneo ambayo jeshi imechukua haijalipa fidia, juhudi zinafanyika ili tuweze kulipa fidia. (Makofi)