Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Primary Question
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Jimbo la Kalambo lina kata 23 na vijiji 111; katika awamu ya kwanza na ya pili ya mradi wa REA ni vijiji vichache tu vilipata umeme. Je, katika utekelezaji wa REA III ni vijiji vingapi vinategemea kupata umeme ili wananchi wa maeneo hayo waweze kujiandaa kujiendeleza kiuchumi?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipatia nafasi niulize swali la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali madogo mawili.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa katika awamu iliyotangulia Wilaya ya Kalambo ilipatia umeme vijiji vichache sana kutokana na scope ya kazi iliyokuwa imetolewa. Je, Serikali ipo tayari kuhakikisha kwamba vile vijiji ambavyo vilikuwa viwe kwenye REA Awamu ya Pili vinaanza kuwekewa umeme haraka iwezekanavyo, ikiwepo kijiji cha Mwazi ambacho tayari transfoma iko pale ni suala la kushusha umeme pamoja na kijiji cha Kazila? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri ni shuhuda, tulienda naye, akaenda kijiji cha Samazi na Ukanda wa Ziwa Tanganyika, miundombinu ya kule alikiri jinsi ambavyo iko haja kubwa ya kuhakikisha kwamba umeme unafika maeneo yale.
Je, yupo tayari kuhakikisha kwamba vijiji hivi vinapatiwa umeme haraka iwezekanavyo?
Name
Dr. Medard Matogolo Kalemani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chato
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Kandege tumetembea naye kwenye Jimbo lake, hakika wananchi wa Jimbo lako Mheshimiwa wanafarijika sana.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na maswali yake mawili ya nyongeza, kweli katika Jimbo la Kalambo ni vijiji 12 tu vilipitiwa na vyenyewe tulipeleka kwenye vituo tu vya umeme, sasa nikuhakikishie Mheshimiwa Kandege, vijiji 89 vyote vilivyobaki, ikiwemo kijiji cha Jengeni, Nondo, Santa Maria, Legeza Mwendo na vingine vyote ninakuhakikishia kwamba vitapelekewa umeme sasa.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali la pili ninahakikisha vipi. Hatua ya kwanza kabisa tumempelekea mkandarasi, hivi sasa Mkandarasi Nakroi ameishaonana na Mheshimiwa Mbunge na ataanza sasa jitihada za kuendelea katika Jimbo lako la Kalambo. Nikuhakikishie kwamba ataanza na maeneo ambayo tayari kuna transfoma kazi iliyobaki sasa ni kuwasha na ataanza na kuwasha. Katika eneo la Santa Maria pamoja na kwamba msishindane na lenyewe itapelekwa transfoma ili umeme uanze kuwaka mara moja. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved