Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Marwa Ryoba Chacha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Serengeti

Primary Question

MARWA R. CHAHA (K.n.y. MHE. SABREENA H. SUNGURA) aliuliza:- Akiwa katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 Mheshimiwa Rais aliahidi ujenzi wa barabara ya lami (Kasulu Road) ili kufungua Mji wa Ujiji:- Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi huo?

Supplementary Question 1

MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, Mheshimiwa Waziri anasema ujenzi unaweza kuanza mwaka 2018/2019, unaweza kuanza. Sasa wananchi wa Mji wa Ujiji na Kasulu kwa ujumla wanataka kupata uhakika, yaani ile commitment ya uhakika kwamba utaanza 2018 au unaweza maana ukisema unaweza, unaweza usianze.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika Mji wa Mugumu tulipewa kilomita mbili mwaka wa fedha uliopita lakini kilomita mbili hizi tumetangaza mara tatu hazijapata mkandarasi kwa sababu ya kilometa chache. Je, Wizara iko tayari kwa mwaka ujao wa fedha kutuongezea kilomita iwe rahisi kwa ajili ya wakandarasi kufanya mobilization?

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tumesema kwamba ujenzi unaweza ukaanza kwa sababu bajeti haijapitishwa na Bunge. Naomba Mheshimiwa Mbunge tushirikiane naye kupitisha kwanza bajeti ndiyo ujenzi uweze kufanyika vinginevyo kama Bunge halitapitisha bajeti hiyo, ujenzi hauwezi kuanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili amesema kwamba wamepata ugumu kupata mkandarasi kwa sababu ya ufupi wa barabara ya kilomita. Ningemwomba Mheshimiwa Mbunge amshauri Mkurugenzi wake wa Halmashauri aweze kutembelea Halmashauri za jirani ambazo zimeweza kujenga hizo hizo kilomita mbili na zimepata wakandarasi. Ahsante sana.

Name

George Malima Lubeleje

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MARWA R. CHAHA (K.n.y. MHE. SABREENA H. SUNGURA) aliuliza:- Akiwa katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 Mheshimiwa Rais aliahidi ujenzi wa barabara ya lami (Kasulu Road) ili kufungua Mji wa Ujiji:- Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi huo?

Supplementary Question 2

MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru sana kwa kunipa nafasi ili na mimi niulize swali moja la nyongeza. Kwa kuwa mwaka 2015 wakati wa kampeni Mheshimiwa Rais alituahidi kilomita10 Mpwapwa Mjini na kwa kuwa bajeti iliyopita tumepewa kilomita moja tu, hata Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Jafo analifahau hilo. Je, Mheshimiwa Waziri ataahidi wananchi wa Mji wa Mpwapwa kwamba hizo kilomita 10 zitakamilika?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nimpongeze Naibu wangu kwa ufafanuzi mzuri wa maswali ya awali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini katika swali la Mheshimiwa Lubeleje, ni kweli anachozungumza na mimi na yeye tulikuwa pamoja pale Mpwapwa Mjini kukagua barabara na ndiyo maana tumempelekea injinia mzuri sana kupitia TARURA na injinia yule wakati tunafanya ukaguzi wa Shule ya Sekondari ya Mpwapwa nilimpa maelekezo maalum.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba nimtoe hofu Mheshimiwa Lubeleje ule ujenzi wa lami unaoendelea pale Mpwapwa Mjini tutaukamilisha na itakapofika 2020 Mheshimiwa Lubeleje awe na uhakika kwamba ahadi ya Mheshimiwa Rais itakuwa imekamilika na kuthibitisha kwamba Mbunge wao amefanya vyema kusimamia eneo hilo. Ahsante sana.

Name

Joseph Osmund Mbilinyi

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Mbeya Mjini

Primary Question

MARWA R. CHAHA (K.n.y. MHE. SABREENA H. SUNGURA) aliuliza:- Akiwa katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 Mheshimiwa Rais aliahidi ujenzi wa barabara ya lami (Kasulu Road) ili kufungua Mji wa Ujiji:- Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi huo?

Supplementary Question 3

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Hizi kilomita 10 Mheshimiwa Rais aliahidi maeneo mengi sana. Nashauri data zote za kilomita 10 ambazo Mheshimiwa Rais aliahidi ili wamkumbushe kwa sababu kwa Jiji langu la Mbeya aliahidi pia kilomita ikiwemo barabara ya Mapelele, Kata ya Ilemi lakini mpaka leo hatuoni mchakato wowote na hatujapata nafasi ya kumuuliza Mheshimiwa Rais kwa sababu hajawahi kuja Mbeya toka amechaguliwa zaidi anarudi tu Kanda ya Ziwa. Mara ya mwisho ilikuwa aje Mbeya juzi kwenye ALAT, lakini waka-cancel siku mbili kabla ya siku ya ALAT kufanyika…
Kwa hiyo, tunamwomba sana Mheshimiwa Rais aje Mbeya pia.

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la rafiki yangu Mheshimiwa Sugu, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tunazo takwimu zote za nchi nzima za ahadi za Mheshimiwa Rais za ujenzi wa miundombinu ya lami lakini na maeneo mengine. Mheshimiwa Sugu anafahamu pale katika Jiji la Mbeya kupitia Ofisi yetu tumepata investment kubwa ya kujenga barabara za lami katika Jiji la Mbeya. Siyo barabara za lami peke yake tumefanya uboreshaji, zile barabara zote tunazifunga taa na kujenga damp za kisasa kupitia mradi wa Strategic City Project.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, jambo hili ni commitment ya Serikali na tumefanya vizuri Jiji la Mbeya, Tanga na Arusha na niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba ahadi zote ambazo Mheshimiwa Rais alizizungumza katika Halmashauri mbalimbali tutazitekeleza kupitia miradi yetu na kuhakikisha kwamba ikifika 2020 viporo hivi tutakuwa tumevimaliza hakuna shida ya aina yoyote.

Name

Mendard Lutengano Kigola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Primary Question

MARWA R. CHAHA (K.n.y. MHE. SABREENA H. SUNGURA) aliuliza:- Akiwa katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 Mheshimiwa Rais aliahidi ujenzi wa barabara ya lami (Kasulu Road) ili kufungua Mji wa Ujiji:- Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi huo?

Supplementary Question 4

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi. Kuna barabara ambazo upembuzi yakinifu ulishakamilika toka mwaka 2015/2016. Kwa mfano, barabara ya kutoka Nyororo - Igohole mpaka Mtwango upembuzi yakinifu ulishafanyika. Ni lini sasa Serikali itaanza utekelezaji wa kujenga barabara ile kwa kiwango cha lami?

Name

Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Kigola anafahamu tulipokuwa Wilayani kwake tulizunguka maeneo mbalimbali na barabara anayoizungumzia ilikuwa ni barabara ya TANROADS na kulikuwa na barabara zingine za Halmashauri ambazo TARURA itashughulikia na zile barabara za Kimkoa ambazo TANROADS itashughulikia. Najua wazi kwamba mazoezi ya upembuzi yakinifu katika maeneo mbalimbali yanafanyika na kwa vile ile ilikuwa katika ahadi na Ilani ya Chama cha Mapinduzi, naomba nimhakikishie kwamba Serikali ni moja, tutahakikisha jukumu la Serikali tunalifanya ili barabara ile ya Nyororo iweze kujengwa kwa kadri iwezekanavyo.