Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Raphael Michael Japhary

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Moshi Mjini

Primary Question

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL aliuliza:- Gereza la Karanga ni chakavu na lina uhaba wa samani:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kulikarabati gereza hilo? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka fedha za kutosha za uendeshaji ili kununua samani pamoja na vifaa vingine vitakavyosaidia kutoa huduma kwa wafungwa na mahabusu gerezani hapo?

Supplementary Question 1

MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, Gereza la Karanga lina tatizo kubwa sana la vyombo vya usafiri kwa maana ya magari. Naomba majibu ya Serikali kwamba ina mpango gani wa kununua gari ili kusaidia wafungwa wanaokata rufaa pamoja na askari ili kulinda usalama wa wafungwa kwa sababu gari lililopo ni chakavu sana na hata matairi halina?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Gereza la Karanga limekuwa na tatizo la madeni makubwa kwa matibabu ya wafungwa wanaotibiwa nje ya zahanati ya gereza hilo. Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba madeni yanayodaiwa gereza yanalipwa ili wafungwa waendelee kupata huduma ya matibabu? Ahsante sana.

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tuna matatizo ya upungufu wa magari katika Jeshi la Magereza maeneo mbalimbali nchini ikiwemo kwenye Gereza la Karanga kiasi tumefikia hatua ya kuweza kufikiria uwezekano kuwapatia magari matano miongoni mwa magari 50 ambayo tunatarajia kuyapokea hivi karibuni kupitia Jeshi la Polisi. Tutalichukua hili suala la Gereza la Karanga tuone kama katika maeneo yaliyo na changamoto kubwa Karanga ni mojawapo ili tuweze kuangalia uwezekano wa kuwapatia gari yatakapokuwa yamewasili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na suala la zahanati, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tunajitahidi kulipia madeni ya magereza ikiwemo zahanati kadri fedha zitakavyokuwa zinaingia. Pia nataka nimkumbushe Mheshimiwa Mbunge kwamba tuna uwekezaji mkubwa katika Gereza la Karanga wa kiwanda chini ya uwekezaji wa Shirika la PPF na moja katika mpango ambao tunataka kutekeleza ni ujenzi wa zahanati kubwa na ya kisasa katika gereza hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti,unaamini kwamba tutakapomaliza ujenzi huo, changamoto hii ya gharama ya matibabu kwa maeneo hayo itasaidia kupatiwa ufumbuzi. Kwa hiyo, nimwombe Mheshimiwa Mbunge aendelee kuvuta subira wakati matatizo haya tunayatatua kwa hatua za muda mfupi na muda mrefu.