Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Tauhida Cassian Gallos Nyimbo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS NYIMBO aliuliza:- Kuna taarifa zilizotolewa na Wizara ya Nishati na Madini za kugunduliwa kwa gesi ya Hellium yenye ujazo wa takribani futi bilioni 54 za ujazo nchini. Je, Serikali imejiandaaje kimkakati kuhusu ugunduzi huo na uchimbaji wa gesi hiyo hasa ikizingatiwa kuwa mataifa makubwa kama Marekani yalishatangaza kukosekana kwa gesi hiyo ifikapo 2030?
Supplementary Question 1
MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS NYIMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa hii ya kumuuliza Mheshimiwa Waziri maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kunijibu swali langu kiufasaha kabisa, lakini vilevile nina maswali mawili madogo.
Je, Serikali inaweza kutuambia nini uchorongaji utafanyika wa kazi hiyo?
Swali langu la pili, je, nje ya Mkoa wa Rukwa kuna Mkoa mwingine wowote umeweza kugundulika kwa gesi hii?
Name
Stanslaus Haroon Nyongo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Mashariki
Answer
NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya uchorongaji itaanza pale taarifa za kijiolojia zikishakamilika na kwa mujibu wa taratibu zilivyokuwa zimepangwa katika Kampuni hii ya Hellium One Tanzania Ltd. wamepanga kuanza shughuli ya uchorongaji kuanzia mwaka 2018.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile swali la pili, ni sehemu gani ambapo hii hellium inapatikana. Kwa kumtaarifu Mheshimiwa Mbunge ni kwamba gesi ya hellium vilevile inapatikana katika Ziwa Eyasi lililoko Mkoa wa Manyara na sehemu nyongine ni sehemu ya Singida ambapo na penyewe inapatikana hii gesi ya hellium. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved