Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Augustino Manyanda Masele
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbogwe
Primary Question
MHE. AUGUSTINO M. MASELE aliuliza:- Katika Wilaya ya Mbogwe kuna Kitalu cha Kigosi North kilichopo katika Pori la Akiba la Kigosi. (a) Je, ni lini Serikali itaanza kulipa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe asilimia 25 ya ada ya uwindaji? (b) Je, ni lini Serikali italitengeneza greda lililoko Kifura Kibondo Makao Makuu ya Mapori ya Kigosi Moyowosi ili lisaidie matengenezo ya barabara ndani ya mapori haya?
Supplementary Question 1
MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri nina maswali mawili madogo ya nyongeza.
Swali la kwanza, Mheshimiwa Naibu Waziri amesema kwamba hiki kitalu kimetolewa kwa ajili mambo ya utafiti wa madini lakini kwa mujibu wa Sheria Na. 5 ya mwaka 2009 ya Wanyamapori inazuia kufanyika kwa utafiti katika maeneo ya hifadhi. Je, ni taratibu zipi ambazo Serikali imetumia kukigawa hiki kitalu ili kifanyiwe mambo ya utafiti wakati sheria hairuhusu?
Swali la pili, kwa kuwa mapori haya yana changamoto mbalimbali, je, Naibu Waziri atakuwa tayari kuambatana na mimi pindi Bunge litakapomaliza shughuli zake ili aweze kuja kuziona hizo changamoto zinazoyakabili haya mapori na kuweza kuzitatua?
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nichukue nafasi hii kumpongeza Mbunge kwa kazi kubwa amekuwa akifanya katika kuwatetea wananchi wake wa Jimbo la Mbogwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu TANZAM ambaye alipewa kitalu hicho, kwa mujibu wa Sheria Na. 5 ya mwaka 2009 kifungu cha 20(2)kinazuia kabisa shughuli zote za utafiti wa madini ya aina zote kufanyika katika maeneo ya hifadhi. Hata hivyo, kifungu hicho cha 20(3)kinatoa mamlaka kwamba ni aina tatu tu za madini zinaruhusiwa kufanyiwa utafiti, madini hayo ni uranium, gesi na mafuta. Kufuatana na mwekezaji aliyekuwa amepewa hiki kitalu yeye alikuwa anafanya utafiti wa madini ya dhahabu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkataba pamoja na leseni ya huyu mwekezaji ilimalizika tereha 31 Desember 2014, baada ya kumalizika, tarehe 1 Juni, 2016 Serikali ilimuandikia barua ya kumuomba aondoke katika eneo na aondoe vitu vyote lakini hadi leo bado mwekezaji yule yupo opale na ameweka vifaa vyake wakati hana leseni na ilishapita. Tarehe 28 Aprili, 2017 alikumbushwa juu ya suala hili na mpaka sasa hivi bado hajasema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie nafasi hii kutoa siku saba, yule mwekezaji aondoe hivyo vitu vyote, kwa sababu viko pale kinyume na taratibu na sheria iliyopo. (Makofi)
Baada ya kumalizika, tarehe 1 Juni, 2016 Serikali ilimuandikia barua ya kumuomba aondoke katika eneo na aondoe vitu vyote lakini hadi leo bado mwekezaji yule yupo opale na ameweka vifaa vyake wakati hana leseni na ilishapita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 28 Aprili, 2017 alikumbushwa juu ya hili suala na mpaka sasa hivi bado hajasema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie nafasi hii kutoa siku saba, yule mwekezaji aondoe hivyo vitu vyote kwa sababu viko pale kinyume na taratibu na Sheria iliyopo. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved