Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Amb. Adadi Mohamed Rajabu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Primary Question

MHE.BALOZI ADADI M. RAJAB aliuliza:- Vitalu vya miti ya tiki – Lunguza Muheza huuzwa kwa njia ya mnada hali inayosababisha viwanda vidogo vidogo vya Muheza kukosa miti. (a) Je, ni lini Serikali itahakikisha wenye viwanda katika maeneo hayo wanapata vitalu ili kulinda ajira za wanavijiji? (b) Je, kwa nini wanaopata vitalu wasichane magogo hayo hapo Wilayani ili kulinda viwanda vidogo vidogo vya Muheza?

Supplementary Question 1

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza utaratibu huo ambao wa kuwauzia watu binafsi kwa makubaliano kwa asilimia 70 na huu wa asilimia 30 kwa kupeleka kwenye mnada hautumiki kabisa. Labda wanatumia asilimia 100 wanapeleka kwenye mnada. Kitendo hiki kimefanya vile viwanda vidogo vidogo Muheza pale, karibu viwanda kumi vyote vimekufa na ajira ambayo kila kiwanda kilikuwa kinachukua labda watu kutoka 100 – 150 wote kukosa kazi.
Sasa nataka kumuuuliza Mheshimiwa Waziri, kwa nini wasirudishe ule utaratibu ambao ulikuwepo wa hiyo asilimia 70 kwa makubaliano ili wale wenye viwanda vidogo vidogo ambao wanatunza ile misitu(tiki) pale waweze kupata ajira na kuendelea kupata morali ya kuanza kutunza?
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ni kwa nini hata wale ambao wananunua kwa mnada ambao utakuta anakuja tajiri mmoja ananunua mitiki yote pale. Sasa ni kwa nini na yeye asilazimishwe kutengeneza kiwanda cha kukata ile mitiki pale pale Muheza kwa sababu hayo ni madaraka ambayo anayo Waziri kufuatana na regulations ambazo anazitengeneza? Nakushukuru Mheshimiwa Waziri.

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa kwamba ukiuza kwa njia ya mnada wananchi wengi wanakuwa hawana uwezo wa kushinda ndiyo maana tumeweka utaratibu kwamba ni asilimia 30 ndiyo itakayouzwa kwenye mnada. Asilimia 30 itategemeana na makubaliano binafsi, maana yake tunafuata bei ile iliyokuwa na mnada, tunaangalia viwanda vyote vilivyoko katika eneo husika. Wale wote wanaohitaji wanapeleka maombi na wanapatiwa ili waweze kujijengea uwezo na kuweza kuzalisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala la pili ambalo amesema kwamba tumshauri huyu atakayekuwa ameshinda aweze kuwekeza katika eneo husika mimi nafikiri ni ushauri mzuri. Tutalifanyia kazi mara tutakapopata muda husika.Ahsante.