Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Kiswaga Boniventura Destery
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Magu
Primary Question
MHE. KISWAGA B. DESTERY (K.n.y. MHE. NJALU D. SILANGA) aliuliza:- Maeneo mengi yamefanyiwa utafiti na kampuni za kigeni kwa muda mrefu bila kufikia hatua ya kufungua migodi. Je, Serikali ina mpango gani wa kuzifutia leseni kampuni hizo na kuwapatia wachimbaji wadogo wadogo?
Supplementary Question 1
MHE. KISWAGA B. DESTERY: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali.
Kwa kuwa Serikali imekiri kufuta leseni 423 yenye eneo la hekta 69,652.88; je, Serikali iko tayari kuwapatia wachimbaji wadogo wadogo eneo hili ambalo limefanyiwa utafiti ili waweze kujiajiri na kujipatia ajira na waweze kulipa kodi stahiki?
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, je, Serikali iko tayari kuwanunulia vifaa vinavyohusiana na wachimbaji wadogo wadogo ili waweze kukodisha kuliko ilivyo sasa wanachimba bila utaalam na vifaa vinavyostahili?
Name
Stanslaus Haroon Nyongo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Mashariki
Answer
NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza ni kwamba Serikali iko tayari kuwasaidia wachimbaji wadogo. Imekwisha kutenga maeneo 11 ambayo yana jumla ya hekari 38.9 kwa ajili ya wachimbaji wadogo wadogo. Kwa hiyo, kwa maeneo haya ambayo yamesharudishwa Serikalini, Serikali itaendelea kufanya mpango wa kuweza kuwapatia wachimbaji wadogo wadogo ili waweze kuchimba na wao waweze kupata faida na waweze kunufaika na madini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, wachimbaji wadogo kupitia ruzuku iliyokuwa inapitia SMMRP ambayo ilikuwa inatoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo na wadau wengine wa uchimbaji iliweza kutoa fedha ili kuweza kuwasaidia wadau waweze kununua vifaa kwa ajili ya uchorongaji, kufanya utafiti na kuweza kusaidia wale wachimbaji wengine wadogo wadogo kwa kukodisha. Lakini vilevile STAMICO ambayo iko chini ya Wizara ya Madini pamoja na GST na yenyewe ina juhudi za dhati kabisa kununua vifaa ambavyo wachimbaji wadogo watakuwa wanakodisha ili waweze kujua mashapu yaliyopo ni mashapu ambayo yana faida ambayo wanaweza wakachimba na wakapata uchimbaji wa tija ili kujiondoa katika ule uchimbaji ambao wanachimba kwa kubahatisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo Serikali iko pamoja na wachimbaji wadogo. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved