Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Mary Michael Nagu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. DKT. MARY M. NAGU aliuliza:- Mwaka 2014/2015 Serikali kupitia Agizo la Mheshimiwa Rais iliwataka wananchi kuchangia ujenzi wa maabara na wananchi waliitikia kwa kiasi kikubwa sana, hasa katika Wilaya ya Hanang:- (a) Je, ni lini Serikali italeta vifaa vya maabara katika majengo hayo ya maabara yaliyokamilika katika Wilaya ya Hanang? (b) Je, Serikali itasaidia vipi kukamilisha maabara ambazo kutokana na njaa wananchi hawakuweza kukamilisha ujenzi wake?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Spika, naomba nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kulifanyia swali langu kazi ya kutosha. Naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kutokana na kutenga Sh.253,913,281/= kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya maabara. Je, ni lini fedha hizo zitatolewa kwa sababu, zikichelewa watoto watakuwa wanakosa masomo ya sayansi ki- practical?
Mheshimiwa Spika, swali lingine dogo la pili ni kwamba, kutokana na kutenga shilingi milioni 70 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara zile ambazo bado hazijakamilika, ningependa kujua kwa dhati kutoka kwa Mheshimiwa Waziri, lini fedha hizo zitatoka? Nami naahidi kuwahamasisha wananchi wa Hanang kujitolea kwa kiasi ambacho kimepangwa?

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba, hiki ambacho kimekusudiwa kwa maana ya kununua vifaa vya maabara na kukamilisha maabara inafanyika kwa wakati. Pindi pesa zitakapokuwa zimekamilika kupatikana hakika nimhakikishie Mbunge kwamba, pesa hizo zitapelekwa. Cha msingi tuhakikishe kwamba, zinafanya kazi iliyokusudiwa.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, majibu yake ni sawa na lile la kwanza.

Name

Omary Tebweta Mgumba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini Mashariki

Primary Question

MHE. DKT. MARY M. NAGU aliuliza:- Mwaka 2014/2015 Serikali kupitia Agizo la Mheshimiwa Rais iliwataka wananchi kuchangia ujenzi wa maabara na wananchi waliitikia kwa kiasi kikubwa sana, hasa katika Wilaya ya Hanang:- (a) Je, ni lini Serikali italeta vifaa vya maabara katika majengo hayo ya maabara yaliyokamilika katika Wilaya ya Hanang? (b) Je, Serikali itasaidia vipi kukamilisha maabara ambazo kutokana na njaa wananchi hawakuweza kukamilisha ujenzi wake?

Supplementary Question 2

MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Kutokana na Sera nzuri ya Serikali ya CCM ya Elimu Bila Malipo imesababisha mwamko wa elimu na wanafunzi kufauli kwa kiasi kikubwa na kusababisha upungufu wa madarasa zaidi ya vyumba 45 katika Jimbo langu. Je, Serikali imejipangaje katika kutatua tatizo hili la ujenzi wa vyumba 45 ukizingatia kipindi hiki wananchi wengi wako kwenye kilimo?

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, upungufu wa vyumba vya madarasa ambavyo vipo kwenye jimbo lake, hakika upungufu huu upo kwenye majimbo mengi. Katika moja ya maswali ambayo nilijibu wakati ameuliza Mheshimiwa Esther Matiko akiwa anaongelea juu ya uhaba wa vyumba vya madarasa, nika- refer kwamba, ni wajibu wetu sisi wananchi kwa kushirikiana na sisi viongozi pamoja na Serikali, kwanza kwa kutazama idadi ya vijana ambao wanajiunga na shule zetu na hasa baada ya mwitikio mkubwa baada ya Elimu Bila Malipo, Sera ambayo inatekelezwa vizuri sana na CCM.
Mheshimiwa Spika, ni wajibu wetu sisi kwa kushirikiana na wananchi tuhakikishe kwamba, kwanza halmashauri zetu ndani ya own source zetu tunatenga na tuwashirikishe wananchi na Serikali nayo itaunga mkono.