Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Halima Abdallah Bulembo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HALIMA A. BULEMBO aliuliza:- Kumekuwa na upandaji holela wa gharama za pango kwa nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Je, Serikali haioni kwamba kuna haja ya kudhibiti upandaji holela wa pango ambao unaathiri wananchi wengi kutokana na kipato chao?
Supplementary Question 1
MHE. HALIMA A. BULEMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba kuuliza swali moja tu la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kati ya asilimia 56 mpaka 60 ya watanzania ni vijana lakini vijana wanashindwa kutimiza malengo yao ama ndoto zao kutokana na gharama kubwa ya upangaji wa nyumba za makazi hasa mijini kuwa kubwa na wamiliki kutaka kupewa kodi za mwaka au miezi sita.
Je, ni lini sasa Serikali itafuta utaratibu huu na sisi kama Bunge tutunge sheria itakayowalazimisha wamiliki wote kupokea kodi ya kila mwezi badala ya mwaka ama miezi sita kama ilivyo sasa? (Makofi)
Name
Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nimpongeze kwa kuona kwamba ipo haja ya kuona kwamba wapangaji wa nyumba wanakuwa na sheria ambayo inasimamia katika suala zima la upangaji. Naomba nimtaarifu Mheshimiwa Mbunge pamoja na Wabunge kwamba Wizara tayari imekwishaliona hilo na tayari tupo kwenye mchakato wa kuanzisha mamlaka itakayosimamia masuala yote ya nyumba. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, katika sheria hiyo ambayo italetwa hapa Bungeni, tumeangalia suala zima la ukomo wa kutoa kodi za nyumba, hiyo ya miezi sita na mwaka mmoja haitakuwepo kwa sababu tumeona inaumiza watu wengi. Kwa hiyo, kodi itakuwa inalipwa kwa mwezi mmoja mmoja na wakati huo huo utatakiwa kuweka kama amana ya miezi mitatu kwa ajili ya shughuli ambazo zinaweza kuwa, kwa hiyo nimesikia na tunalifanyia kazi. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved