Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ignas Aloyce Malocha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Primary Question

MHE. IGNAS A. MALOCHA aliuliza:- Katika ukanda wa Bonde la Ziwa Rukwa katika Jimbo la Kwela, kwenye ukingo wa Milima ya Lyamba Iyamfipa inayoambaa katika Kata za Mfinga, Mwadui, Kalumbaleza, Nankanga, Kapeta hadi Kaoze, baadhi ya wananchi wamekuwa wakiokota madini mbalimbali bila kutambua ni madini ya aina gani. (a) Je, Serikali imeshafanya utafiti wowote katika maeneo hayo? (b) Kama jibu ni hapana, je, ni lini utafiti utafanyika ili kujua eneo hilo lina madini gani?

Supplementary Question 1

MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kushika nafasi hiyo mpya na kwa kweli ameanza kuifanya vizuri Mwenyezi Mungu aendelee kumuongoza aendelee kuifanya vizuri zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ninayo maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza sisi sote tunafahamu wazi kwamba maeneo yaliyo na madini yanatoa fursa kwa vijana wengi kujiajiri kwa machimbo madogo madogo kwa kujipatia kipato na vilevile Serikali kukusanya kodi. Tunafahamu kwamba Serikali ilishafanya utafiti katika maeneo mengi, lakini utafiti huo uko ndani ya vitabu mpaka uende maktaba jambo ambalo sio rahisi wananchi wa kawaida vijijini kutambua wapi kuna madini.
Mheshimiwa Naibu Spika, je, kwa nini Serikali isiainishe maeneo yote yenye madini kwa uwazi ili wananchi waweze kuyatambua na kufanya kazi ya uchimbaji mdogo mdogo?
La pili umesema kwamba wananchi wanaweza kutumia ofisi za kanda za Magharibi zilizopo Mpanda na Dodoma, jambo ambalo ni vigumu kwa wananchi wa kawaida hasa wa vijijini kuzitumia ofisi hizo kutokana na umbali uliopo. Kwa nini Serikali isiweke branch katika mikoa yote ili kurahisisha wananchi kuzishilikia ofisi hizo?

Name

Doto Mashaka Biteko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukombe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MADINI (MHE. DOTTO M. BITEKO):
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ijulikane tu kwamba matumizi ya ofisi zetu za Wakala wa Jiolojia ni matumizi ambayo yanawahusu Watanzania wote. Ni bahati mbaya tu kwamba wageni wanaotoka nje kuja kutafuta madini hapa nchini wao wanazitumia zaidi ofisi hizi kuliko sisi Watanzania.
Naomba nitoe wito sasa kwa Watanzania wote tuzitumie Ofisi zetu hizi za Wakala wa Jiolojia ili ziweze kutusaidia katika sekta hii ya madini.
Lakini la pili kwa nini Serikali sasa isiweke branch kwa kila Wilaya na kila maeneo. Naomba nimuombe Mheshimiwa Malocha, na kwasababu amekuwa mdau mkubwa sana wa kufuatilia jambo hili kwaajili ya wananchi wake; sisi ni watumishi wa wananchi, sisi hatukai ofisisni Mheshimiwa Malocha ukiwahitaji wataalamu wetu wa Jiolojia kuja kwenye eneo lako wakati wowote watakuja, na hata kama utamuhitaji Waziri mwenyewe atakuja kwasababu sisi ni watumishi wa wananchi.