Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Ally Yusuf Suleiman

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Mgogoni

Primary Question

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF aliuliza:- Kuna ushahidi wa kutosha kwamba kuna watu kadhaa ambao wamekuwa wakikamatwa na Jeshi la Polisi Unguja na Pemba huku baadhi yao wakifunguliwa mashtaka na wengine kuachiwa:- (a) Je, ni kwa nini Jeshi la Polisi linashindwa kufanya kazi kwa weledi na kukamata watu pasipo ushahidi kwa lengo la kukomoa tu? (b) Ili kulisafisha Jeshi la Polisi, je, Serikali haioni haja ya kuwawajibisha watendaji ambao wenye tabia ya kuwakomoa wananchi kwa kuwakamata pasipo ushahidi?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF: Mheshimiwa Naibu wa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Katika jawabu la msingi la Mheshimiwa Waziri amesema Jeshi la Polisi limepewa mamlaka kisheria kutuhumu, kukamata, kuhoji na kuweka watuhumiwa mahabusu kwa muda ulioruhusiwa kisheria.
Mheshimiwa Naibu Spika, wako watu wengi ambao wanawekwa mahabusu ya polisi kwa zaidi ya siku 15, akiwemo mwanafunzi Abdul Nondo, ambao wanawekwa mahabusu ya polisi kwa zaidi ya siku 15 bila ya kupelekwa mahakamani. Nataka nijue ni sheria gani ambayo inatumika au inatumiwa na polisi kuwaweka watu mahabusu ya polisi kwa muda huo mrefu bila ya kuwapeleka mahakamani? Nataka kujua sheria ni sheria gani. Swali la kwanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, ni hatua gani ambayo Mheshimiwa Waziri ataichukua iwapo tutamletea orodha ya watu ambao wamebambikiziwa kesi?

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama nilivyosema jeshi la polisi linafanya kazi kwa mujibu wa sheria na katika ufanyaji kazi wake kuna hatua mbalimbali za kuchukua ikiwemo kufanya upelelezi, kufanya mahojiano na baadaye mambo yote yale yakikamilika hatua nyingine ndipo huwa zinafuatia.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa jambo la usalama ni kipaumbele, usalama wa mtuhumiwa lakini na usalama wa raia wengine wanaosalia, Jeshi la Polisi hutumia wajibu wake lililopewa wa kulinda usalama wa raia kuweza kuhakikisha kwamba linatimiza majukumu yake na huku watu wakiwa salama pamoja na mali zao.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu jambo la pili, kwa kuwa ni suala la takwimu nitamwomba Mheshimiwa Mbunge niweze kuwasiliana naye kuweza kumpa masuala yale ya takwimu na yeye kama ana orodha kuweza kubadilishana orodha hizo. Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru.

Name

Khatib Said Haji

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Konde

Primary Question

MHE. DKT. SULEIMAN ALLY YUSSUF aliuliza:- Kuna ushahidi wa kutosha kwamba kuna watu kadhaa ambao wamekuwa wakikamatwa na Jeshi la Polisi Unguja na Pemba huku baadhi yao wakifunguliwa mashtaka na wengine kuachiwa:- (a) Je, ni kwa nini Jeshi la Polisi linashindwa kufanya kazi kwa weledi na kukamata watu pasipo ushahidi kwa lengo la kukomoa tu? (b) Ili kulisafisha Jeshi la Polisi, je, Serikali haioni haja ya kuwawajibisha watendaji ambao wenye tabia ya kuwakomoa wananchi kwa kuwakamata pasipo ushahidi?

Supplementary Question 2

MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Napenda kumuuliza Mheshimiwa Waziri, ni muda gani kisheria jeshi la polisi linaposhindwa kupeleka ushahidi wa kesi unaopeleka mahakamani naweza kupeleka maombi ya kuondoa mashitaka hayo mahakamani?

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumjibu ndugu yangu Khatib wa kutoka kwetu kule kwa mama, kwamba makosa ya jinai hayana ukomo kwa hiyo, inategemea kosa analolisemea ambalo anaweza akasubiria na akaenda kuomba liondolewe ni aina gani ya makosa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maana hiyo kama makosa ni yale ambayo shitaka lake halina ukomo, basi ni vyema kuacha vyombo vingine ambavyo vinatoa hukumu vikatoa hukumu ndipo yeye akatambua kwamba jambo hilo limeshafika ukomo. Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.