Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mahmoud Hassan Mgimwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Primary Question
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA (K.n.y. MHE. DEO K. SANGA) aliuliza:- Serikali iliahidi kufuta Ushuru mdogo mdogo unaokusanywa na Halmashauri ili wajasiriamali wadogo wakiwemo akina mama lishe waweze kuongeza kipato kupitia shughuli zao. Je, ni lini Serikali itatoa tamko rasmi kwa Halmashauri zetu nchini ili wasikusanye tena ushuru huo?
Supplementary Question 1
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hii kuipongeza sana Serikali kwa majibu mazuri lakini nina swali la nyongeza.
Pesa hizi zilizokuwa zinakusanywa na Halmashauri zilikuwa zinasaidia kazi ndogo ndogo kwenye zile Halmashauri. Namuomba Mheshimiwa Naibu Waziri atuambie Serikali imepanga vipi kuhakikisha inaziba hilo gap?
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Halmashauri mwanzo zilikuwa zinajielekeza kwa kukusanya tozo hizi ambazo zilikuwa zinasaidia katika kuendesha Halmashauri. Nadhani hiki kilikuwa ni kilio cha Watanzania wote, ambao Watanzania wadogo wadogo kule chini ilikuwa inapigwa kelele sana ndio maana Serikali sasa imeomua kulichukua hili na Wizara ya Fedha hapo alipoweka hotuba yake hapa nilizungumza hili wazi. Kwa hiyo, naomba tukifika katika Finance Bill mtaona jinsi gani Serikali imejipanga na ku-address jambo hilo vizuri kwa mustakabali wa Halmashauri zetu unavyoenda.
Name
Susan Anselm Jerome Lyimo
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MAHMOUD H. MGIMWA (K.n.y. MHE. DEO K. SANGA) aliuliza:- Serikali iliahidi kufuta Ushuru mdogo mdogo unaokusanywa na Halmashauri ili wajasiriamali wadogo wakiwemo akina mama lishe waweze kuongeza kipato kupitia shughuli zao. Je, ni lini Serikali itatoa tamko rasmi kwa Halmashauri zetu nchini ili wasikusanye tena ushuru huo?
Supplementary Question 2
MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Mweyekiti, nakushukuru, pamoja na Serikali kuamua kuondoa tozo hizo tayari Halmashauri zilishaweka kwenye bajeti zao. Je, Serikali inatoa tamko gani ama wata-review hizo bajeti au itakuwaje? Hiyo ndiyo shida yangu ahsante na shida kwenye Halmashauri zetu.
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani hii ni hofu ya Wabunge wengi humu ndani, na hata juzi Wabunge wengi walikuwa wananiuliza kule kwamba jinsi gani tunavyokuja. Na ndiyo maana naomba niwaambie kuwa Serikali itakachokifanya sasa hivi ndiyo maana nimesema tukifika katika Finance Bill tutaona jinsi gani mchanganuo utakavyokwenda. Lengo kubwa kwa sababu Halmashauri zimeshatenga bajeti yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia bajeti ya Halmashauri ilivyotengwa kuna tofauti sasa na kama ambavyo vingine viliwekwa kama ni vyanzo vya mapato katika Halmashauri hiyo. Ndiyo maana Wizara ya Fedha itakapohitimisha mijadala hii tutaona ni jinsi gani mafungu hayo yatawekwa vizuri. Lengo kubwa bajeti ya Halmashauri kama property tax ilivyowekwa katika suala la majumba, kwa hiyo, msihofu katika hili.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved