Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ally Seif Ungando
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibiti
Primary Question
MHE. ALLY S. UNGANDO aliuliza:- Ufunguzi wa Kituo cha Afya Mbwera ulifanyika tarehe 27/8/1994 na aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, wakati huo Dkt. John Samwel Malecela lakini hadi sasa kituo hicho hakina hadhi hiyo ya kuitwa Kituo cha Afya. (a) Je, Mheshimiwa Waziri mwenyewe haoni haja ya kwenda Mbwera kuona hali halisi ya kituo hicho baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wataalamu wake kuona kama kimekamilika? (b) Je, ni lini Serikali itapeleka watumishi wa kutosha kwani wanaotakiwa ni 39 na sasa waliopo ni wanne tu?
Supplementary Question 1
MHE. ALLY S. UNGANDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.
Moja, kwa kuwa kila penye mafanikio hapakosi kuwa na changamoto, je, Waziri sasa yuko tayari kufuatana na mimi kwenda Kituo cha Afya Mbwera kwenda kubaini baadhi ya changamoto za huu ujenzi unaoendelea hivi sasa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwamba hali ya Kituo cha Afya Kibiti majengo yake kwa kweli uchakavu wake hauridhishi. Je, ni lini sasa Serikali itatoa fedha ya kufanya ukarabati Kituo hiki cha Afya Kibiti ili kiweze kutoa huduma yenye tija kwa wananchi wa Kibiti?
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ungando Mwenyekiti wa Wandengereko (a) na (b) kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niko tayari kwa sababu wanasema seeing is believing kama ambavyo juzi nilipata fursa ya kwenda Dar es Salaam kutembelea Kituo cha Afya Buguruni na kule inakojengwa Hospitali ya Wilaya kwa Mheshimiwa Waitara, niko tayari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na kukarabati kituo kingine cha afya ambacho Mheshimiwa Mbunge anaomba, ni dhamira ya Serikali kuhakikisha kwamba tunakamilisha na kukarabati vituo vya afya vingi kadri iwezekanavyo ili kusogeza huduma ya afya na hasa afya ya mama na mtoto kwa kadri itakavyowezekana. Kwa hiyo, kadri bajeti inavyoruhusu naomba nimhakikishie Mbunge kwamba ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba ukarabati unafanyika.
Name
Kasuku Samson Bilago
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Buyungu
Primary Question
MHE. ALLY S. UNGANDO aliuliza:- Ufunguzi wa Kituo cha Afya Mbwera ulifanyika tarehe 27/8/1994 na aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, wakati huo Dkt. John Samwel Malecela lakini hadi sasa kituo hicho hakina hadhi hiyo ya kuitwa Kituo cha Afya. (a) Je, Mheshimiwa Waziri mwenyewe haoni haja ya kwenda Mbwera kuona hali halisi ya kituo hicho baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wataalamu wake kuona kama kimekamilika? (b) Je, ni lini Serikali itapeleka watumishi wa kutosha kwani wanaotakiwa ni 39 na sasa waliopo ni wanne tu?
Supplementary Question 2
MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kituo cha Afya Kakonko kimeelemewa sana na wagonjwa. Kituo hiki cha Afya Kakonko Waziri wa TAMISEMI akiwa Naibu Waziri, Mheshimiwa Jafo, aliwahi kukitembelea akaona ukubwa wa kazi inayofanyika katika kituo kile. Kinapata mgao wa dawa sawa na Kituo cha Afya, kinatoa huduma kama Hospitali ya Wilaya. Sasa ni lini Serikali kwa makusudi kabisa itajenga Hospitali ya Wilaya ya Kakonko ili kuondoa mzigo kwenye Kituo cha Afya cha Kakonko? Ahsante.
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba maeneo yote ambayo kuna Vituo vya Afya na hakuna Hospitali za Wilaya, hivyo Vituo vya Afya ndivyo ambavyo vimekuwa huduma kama Hospitali za Wilaya. Ni ukweli usiopingika kwamba sifa ya kituo cha afya na sifa ya Hospitali ya Wilaya ni tofauti. Ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba maeneo yote ambayo hakuna Hospitali ya Wilaya tunajenga na ndio maana tumeanza na hizo hospitali 67. Ni azma kuhakikisha Wilaya zote Tanzania zinakuwa na Hospitali za Wilaya.
Name
Joseph Leonard Haule
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Mikumi
Primary Question
MHE. ALLY S. UNGANDO aliuliza:- Ufunguzi wa Kituo cha Afya Mbwera ulifanyika tarehe 27/8/1994 na aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, wakati huo Dkt. John Samwel Malecela lakini hadi sasa kituo hicho hakina hadhi hiyo ya kuitwa Kituo cha Afya. (a) Je, Mheshimiwa Waziri mwenyewe haoni haja ya kwenda Mbwera kuona hali halisi ya kituo hicho baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wataalamu wake kuona kama kimekamilika? (b) Je, ni lini Serikali itapeleka watumishi wa kutosha kwani wanaotakiwa ni 39 na sasa waliopo ni wanne tu?
Supplementary Question 3
MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Afya cha Ulaya kinatumika kwa wananchi wote wa Kata za Zombo, Muhenda pamoja na Ulaya, lakini kina upungufu mkubwa sana wa watumishi na hali mbaya sana ya miundombinu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itatupia macho kwenye Kituo cha Afya cha Ulaya ili wananchi wa pale kwenye Tarafa ya Ulaya waweze kupata tiba bora kwa mama na watoto, ahsante.
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH S. KANDEGE) Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati mbaya hicho Kituo cha Afya ambacho Mheshimiwa Mbunge anakitaja cha Ulaya sijapata fursa ya kukitembelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo ni ukweli usiopingika kwamba miongoni mwa mikoa ambayo imepata Vituo vya Afya vya kutosha katika awamu hizi ni pamoja na Mkoa wa Morogoro pamoja na Hospitali ya Wilaya. Ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba Vituo vya Afya vyote ambavyo vinafanya kazi kama Vituo vya Afya, lakini havina hadhi ya Vituo vya Afya tunaenda kuvikarabati na kuviboresha ili vifanane na hadhi ya Vituo vya Afya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ni azma ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli na yeye na pale alichombeza akaimba na wimbo nina amini hatutamsahau.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA): Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote naomba uniruhusu niwape pole sana wenzetu wa Yanga kwa sababu msiba wa jirani yako ni msiba wa wote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba asiwe na wasiwasi, naomba awe na subira mwaka 2018/2019 hii inakuja tutashughulikia suala lake la Ulaya.
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. ALLY S. UNGANDO aliuliza:- Ufunguzi wa Kituo cha Afya Mbwera ulifanyika tarehe 27/8/1994 na aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, wakati huo Dkt. John Samwel Malecela lakini hadi sasa kituo hicho hakina hadhi hiyo ya kuitwa Kituo cha Afya. (a) Je, Mheshimiwa Waziri mwenyewe haoni haja ya kwenda Mbwera kuona hali halisi ya kituo hicho baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wataalamu wake kuona kama kimekamilika? (b) Je, ni lini Serikali itapeleka watumishi wa kutosha kwani wanaotakiwa ni 39 na sasa waliopo ni wanne tu?
Supplementary Question 4
MHE. BONIPHACE P. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, asante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza…
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna ujenzi wa Vituo vya Afya katika nchi yetu kwa maeneo mbalimbali. Kuna vituo vimepata shilingi milioni 500 na kuna vituo vimepata shilingi milioni 400. Sasa huwa najiuliza na wanasema vituo vyote vimepata shilingi milioni 700; shilingi milioni 200 kwa vituo vilivyopata shilingi milioni 500 inaenda MSD na shilingi milioni 300 kwa vituo vilivyopata shilingi milioni 400 imeenda MSD. Sasa huwa najiuliza…
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii tofauti ya fedha za kwenda kununua vifaa MSD ya shilingi milioni 300 na shilingi milioni 200 na shirika ni lile lile, la Serikali tofauti yake inatokana na nini? Ahsante. (Makofi)
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, swali hili linajirudia kwa mara nyingine na nikiwa hapa niliwahi kutoa ufafanuzi kwamba kwanza inategemeana na source of fund; kuna maeneo mbalimbali ambayo tumepata fedha.
Kwa hiyo, inategemea shilingi milioni 500 au shilingi milioni 400, kama ni Benki ya Dunia, Canada, Serikali ya Tanzania lakini pia inategemeana na hali ya Kituo cha Afya husika kwa sababu kuna baadhi ya Vituo vya Afya vinahitaji ukarabati mdogo, vingine ukarabati wake ni mkubwa. Kwa hiyo, tumekuwa tukifanya scope kujua uhalisia ili Kituo cha Afya kiweze kukamilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na suala zima la pesa ambazo zinapelekwa MSD, majibu yake hayana tofauti sana na hili jibu la mwanzo kwa sababu ukienda Kituo cha Afya Manyamanyama ambacho labda kina x–ray center haiwezi kuwa sawa na kituo cha afya kingine ambacho hakina mashine kama hiyo.
Kwa hiyo, Serikali tumekuwa tukiyazingatia hayo wakati tunapeleka fedha, ahsante. (Makofi)