Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Jasson Samson Rweikiza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Vijijini
Primary Question
MHE. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza:- Tanzania haijaidhinisha na kujiunga rasmi na mkataba wa kupambana na silaha za sumu (Biological Weapons Convention):- (i) Je, kwa nini Tanzania haijajiunga na mkataba huo? (ii) Je, Serikali inafahamu madhara ya kutoidhinisha rasmi mkataba huo?
Supplementary Question 1
MHE. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Waziri kwa majibu mazuri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, nchi zinazotuzunguka, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, Zambia, Malawi na Msumbiji wote wameridhia mkataba huu. Kama alivyosema Mheshimiwa Waziri kwenye jibu lake ni nchi sita tu duniani ambazo hazijaridhia na sisi Tanzania tukiwemo. Je, Serikali haioni kwamba ni aibu kubwa sana Tanzania kuwa kwenye kundi hili dogo la nchi sita ambazo zina matatizo ya ndani ambao hazikaridhia mkataba huu za kina Haiti na nyingine hizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, Serikali ipo tayari kutoa ratiba (timeframe) ya kupitia kumaliza mchakato huu wa mkataba huu Serikalini na hatimaye kwenye Bunge hili kabla haujakwisha mwezi wa Juni au Septemba angalau mkataba huu uje Bungeni hapa kwa ajili ya kuridhiwa? (Makofi)
Name
Dr. Hussein Ali Mwinyi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwahani
Answer
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi, haikuonekana sababu wakati ule kwa sababu bila ya kuwa tumeridhia tuliweza kufanya shughuli zetu zote bila ya matatizo yoyote; lakini kwa sasa hivi sababu ipo. Kama nilivyosema kwenye jibu la msingi ni kutokana na matukio ya kigaidi suala hili sasa limefikia wakati muafaka turidhie ili tuondokane na kuwa katika nchi chache ambazo hazijaridhia kama nilivyosema. Ndiyo maana tumeshatayarisha waraka kwa madhumuni ya kupita katika ngazi za maamuzi ili hatimaye uletwe hapa kwa kuridhia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili la timeframe, ninachoweza kusema ni kwamba, utaratibu ni kwamba waraka ukishakamilika una hatua tatu; ya kwanza ni Cabinet Secretariat ambapo unajadiliwa na baadaye IMTC na hatimaye unapita kwenye Baraza la Mawaziri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ni matumaini yangu kwamba hatua hizi tatu zitafanyika kwa haraka ili tuweze kukamilisha suala hili na mkataba huu uridhiwe. Ningependa nimwarifu Mheshimiwa Rweikiza kwamba, kwa Bunge hili tutakuwa tumechelewa, lakini huenda Septemba tukaweza kufanya shughuli hii ikakamilika.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved