Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Khatib Said Haji
Sex
Male
Party
CUF
Constituent
Konde
Primary Question
MHE. KHATIBU SAID HAJI aliuliza:- Mheshimiwa Spika, Sheria za FIFA zimekataza mambo yanayohusiana na mchezo wa soka kupelekwa Mahakamani:- (a) Je, Serikali inatoa tamko gani juu ya makosa yanayofanyika katika klabu za soka? (b) Je, ni kwa kiasi gani sheria hizi za FIFA zinakinzana na Sheria za nchi yetu?
Supplementary Question 1
MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante. FIFA inaitambua TFF kuwa ndio chombo chenye mamlaka ya kusimamia mchezo wa soka Tanzania.
Je, TFF ni Tanzania Football Federation au TFF ni Tanganyika Football Federation? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kama jibu ni Tanzania Football Federation; je, TFF ina mamlaka gani juu ya chombo cha ZFA kule Zanzibar? Kama jibu ni Tanganyika Football Association; ni kwa nini hamjaiandikia FIFA na kuiambia kwamba ZFA haihusiki na mambo ya Chama cha Soka cha Tanzania? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, tatizo la baadhi ya viongozi kule Zanzibar kutotii sheria za nchi siyo tu liko kwenye mambo ya siasa, sasa limehamia mpaka kwenye mambo ya michezo. Hivi tunavyozungumza Makamu Mwenyekiti wa ZFA amekipeleka Mahakamani Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA), jambo ambalo FIFA wakiamua kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria zao, ni kwamba Tanzania itafungiwa uanachama muda wowote kuanzia sasa.
Je, Serikali inatoa tamko gani juu ya viongozi wa vyama vya soka wasiotii na kuheshimu sheria zilizowaweka kwenye madaraka yao?
Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)
Name
Nape Moses Nnauye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtama
Answer
WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, WASANII NA MICHEZO: Mheshimiwa Spika, la kwanza, TFF ni Tanzania Football Association na siyo Tanganyika Football Association. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Spika, ni Tanzania Football Federation na mamlaka yake yanakwenda mpaka Zanzibar… (Kicheko/Makofi)
SPIKA: Jamani, mbona Mheshimiwa Nape akiongea mnachemka sana upande wa pili? (Kicheko/Kelele)
Mheshimiwa Nape, endelea kujibu maswali.
WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI. WASANII NA MICHEZO: Wanajua mimi kiboko yao! (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, ameuliza na ametoa mfano wa viongozi ambao wamepeleka masuala ya michezo Mahakamani. Taratibu za michezo duniani zinajulikana; na kama kuna watu wamepeleka michezo Mahakamani, kwa kweli hukumu yake kwa FIFA inajulikana. Kwa hiyo, tutachukua hatua tuangalie namna ambayo watarudi kwenye utaratibu wa kawaida ili kuepusha kuchukuliwa hatua za kufungiwa michezo.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved